Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko CCM yataka viingilio Sabasaba vipunguzwe
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yataka viingilio Sabasaba vipunguzwe

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Uwanja wa Sabasaba
Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wametakiwa kuangalia upya viingilio vinavyotozwa kwenye maonesho hayo ili kila Mtanzania aweze kushiriki. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam …  (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 6 Julai, 2022 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye Viwanja vya Julius Nyerere Sabasaba wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam.

Shaka alisema CCM wameiona hiyo changamoto na wametoa maelekezo kwa mamlaka husika kufanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha katika maonesho yajayo inatatuliwa.

Alisema matarajio ya CCM ni kuona maonesho hayo ambayo yamekuwa na mvuto duniani kote yanaakisi uhalisia wa maonesho, hali ambayo itatoa fursa kwa kila Mtanzania kuwa na uhuru kushiriki.

“Nikiri inawezekana bei ya kiingilio Sabasaba ni kubwa kwa baadhi ya wananchi, nafikiri wizara na mamlaka husika kuna haja ya kutathmini mapungufu na sisi tumeshaishauri wizara kuangalia eneo hilo ili mwakani kuwe na mazingira rafiki kwa kila mshiriki,” alisema.

Awali alisema pamoja na changamoto hiyo ya bei ya kiingilio, mwitikio wa wafanyabiashara umekuwa mkubwa hali ambayo inaakisi namna Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali wameweza kuimarisha na kuboresha mazigara ya biashara na uwekezaji nchini.

“Ushahidi umeonekana katika Mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo makusanyo ya mapato yalikuwa Sh. trilioni 22.28 ikiwa ni ongezeko la sawa na asilimia 113 ya lengo ukilinganisha na makusanyo ya Sh. trilioni 18.15 mwaka wa fedha 2020/2021.

Chama kimeelekeza katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ibara 49 kwamba Serikali itakazounda zitaboresha mazingira na mifumo ya biashara nchini, ili kuzalisha fursa za ajira na kuongeza mapato ya serikali,” alisema.

Katibu huyo alisema kinachoonekana kwa sasa ni ushahidi tosha kuwa Rais Samia amerejesha imani kwa wafanyabishara, hali ambayo inawavutia kulipa kodi.

“Mafanikio hayo yako kwenye uwekezaji pia, kwani wawekezaji wameongezeka ambapo hadi Mei mwaka huu 2022 uwekezaji ulifikia dola za Marekani bilioni 3 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa tangu tupate uhuru,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tantrade Latifa Khamis alieleza katika maonesho ya mwaka huu makampuni ya kibiashara toka hapa nchini ni takribani 3,000 na kampuni za kibiashara kutoka nje ni 22 ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na maonesho yaliyopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

error: Content is protected !!