August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

10,000 wafariki vita ya Urusi, Ukraine

Spread the love

 

WATU takribani 10,000 wameripotiwa kufariki dunia nchini Ukraine, tangu ilipovamiwa kijeshi na Urusi mwishoni wa Februari, 2022, ambapo Umoja wa Mataifa (UN) umesema kati ya vifo hivyo, raia 4,700 Ukraine wamepoteza maisha. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, vifo hivyo vimetokea kuanzia Februari hadi Juni mwaka huu, huku ukieleza kwamba takwimu hizo ni pungufu ikilinganishwa na idadi halisi ya vifo kutokana na changamoto ya ukosefu wa idadi kamili kutokana na mapigano ya kijeshi yanayoendelea.

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu nchini Ukraine, Matilder Bogner, amesema raia waliofariki dunia walikuwa katika miji iliyozingirwa au inayogombaniwa kwa sababu walikosa huduma z matibabu na msongo wa mawazo.

Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na BBC Swahili, watu wengi wamepoteza maisha katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv, wakati ulipozingirwa na vikosi vya kijeshi vya Urusi.

Wakatri takwimu hizo zikitolewa, Msaidizi Mkuu wa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, alisema wanajeshi wa taifa hilo kati ya 100 hadi 200, hupoteza maisha kila siku.

Pia, Urusi imesema imeua wanajeshi wa Ukraine zaidi ya 20,000, huku wanajeshi wake 1,351 wakipoteza maisha tangu vita hiyo ianze.

error: Content is protected !!