August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rwanda, Congo wakubaliana kumaliza tofauti zao

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto), João Lourenço wa Angola (katikati) na Félix Tshisekedi wa Kongo wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wao wa tatu kutafuta suluhu mjini Luanda.

Spread the love

 

JAMHURI ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda zimekubaliana kuanza mchakato wa kumaliza tofauati zao, baada ya mkutano wa marais wa nchi hizo mbili waliokutana jana tarehe 6 Julai, 2022 jijini Luanda nchini Angola. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Msuluhishi wa mvutano wa wiki kadhaa kati ya nchi hizo jirani, Rais wa Angola, Joao Lourenco, ametangaza kuwa pande mbili zimekubaliana kusitisha mvutano kati, bila ya kueleza kwa undani wa kilichoafikiwa.

Hata hivyo, Ofisi ya Rais Felix Thisekedi, kupitia msemaji wake Erick Nyindu amesema watahakikisha makubaliano yalioafikiwa yanatekelezwa kwa lengo la kupata amani Mashariki mwa DRC na kwamba kuna matumaini uhusiano kati ya Rwanda na DRC utaimarika tena.

Nyindu ameongeza kuwa DRC, itahakikisha wakimbizi hasa wa FDLR na wengine wanarudi wanarejeshwa Rwanda.

Aidha, ripoti zinaeleza kuwa mkutano huo ulikuja na mambo sita ambayo nchi hizo zinataka yatekelezwa ikiwemo kurejesha uhusiano wa kidiplomasia lakini pia kuacha kutumia makundi ya waasi ya M 23 na FDLR kutishia usalama wa nchi hizo mbili.

Kamati ya pamoja kati ya DRC na Rwanda itaundwa kuhakikisha uteketelezwaji wa mambo yaliyokubaliwa na inatarajiwa kukutana jijini Luanda tarehe 12 mwezi huu.

error: Content is protected !!