Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sh trilioni 70 kujenga mradi wa gesi, ajira 10,000 kuzalishwa
Habari za Siasa

Sh trilioni 70 kujenga mradi wa gesi, ajira 10,000 kuzalishwa

Moja ya kituo cha gesi asilia
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa sekta binafsi, taasisi za Serikali na wakuu wa mikoa ya Mtwara na Lindi kujiandaa kutumia fursa zitakazopatikana katika ujenzi wa mradi wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia (LNG). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema mradi huo utatekelezwa kwa thamani ya zaidi ya Sh trilioni 70 huku asilimia 10 ya fedha hizo ambazo ni sawa na Sh trilioni saba zikitarajiwa kutumiwa ndani ya nchi wakati wa ujenzi wa mradi huo utakapoanza.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Juni, 2022 Ikulu Chamwino jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya awali ya mkataba wa kuchakata gesi asilia.

Amesema katika ujenzi wa mradi huo, ajira zaidi ya 10,000 zitapatikana hivyo ni vema taasisi za serikali, wakuu wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuwaanda wananchi wenyeji wa mikoa hiyo kufaidika na fursa zitakazotokana na mradi huo.

Amesema mradi huo utaleta mapato mengi nchini kwani utakapomilika utabadilisha taswira ya uchumi wa Taifa.

Kutokana na hali hiyo ametoa maelekezo matatu kwa Serikali na wadau wengi ili kufaidika na mradi huo.

Mosi ameagiza kikosi cha mazungumzo ya mradi huo kuendelea kusimamia masilahi ya nchi kwenye hatua zifuatazo za mazungumzo.

“Lakini ni muhimu kutambua haya ni majadiliano huwezi kila kitu unachotaka na upande wa pili. Nawasihi tujipe flexibilities.

“Pili, mikoa ya Lindi na Mtwara kunakotekelezwa lazima waone manufaa ya mradi huu.

“Tatu, mchakato wa majadiliano kuhusu maandalizi lazima yapelekee kujenga uwezo wa watanzania ili vizazi vijavyo viweze kuvuna kwa tija zaidi katika mradi huu,” amesema.

Amesema lazima waanze kujenga uwezo wa watanzania kushiriki kikamilifu katika biashara na uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi kwa sababu ni sekta kubwa.

Amesema vilevile panahitajika uimarishaji wa taasisi za umma hususani upande wa sheria, kodi na ulinzi kwani walindaji wa mradi huo ni Watanzania si wawekezaji.

Pia ameagiza TPDC ambao ni wabia wa mradi huo kuwa shiriki la kimkakati kwa nchi ili miaka ijayo lisimame lenyewe kwenye biashara hiyo.

“Ninaomba watanzania waanze kujipanga sasa kwani mbali na mtambo wa kuchakata gesi na shughuli zake kutakuwa na special economic zone, sekta binafsi ijipange sasa kuchukua huduma kwenye huu mradi, tuhudumie mradi huu sisi wenyewe ili tuweze kukuza uchumi wetu wa ndani kuliko waje watu wa nje kutoa huduma kwenye mradi,” amesema.

Amesema maamuzi ya mwisho ya uwekezaji katika mradi huo yanatarajiwa kufikiwa mwaka 2025.

“Kwa hiyo kusaini kwetu hapa haina maana tutaanza uwekezaji kesho, bado kuna mengi ya kuzungumzwa katika vipengele kadhaa vya kukubaliana, bado kuna vipengele vinahitaji mjadala, matumaini yetu ikifika Disemba tusaidi mkataba wa pili ambao tutakuwa tumemaliza kwenye awamu ya kwanza ya majadiliano ambapo itaruhusu kuanza awamu ya pili, nawahimiza mmalize mapema,” amesema.

Rais Samia amemshuhudia Waziri wa Nishati, Januari Makamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC), Dk. James Matarajio wakitia saini kwa upande wa Serikali na upande wa makampuni ya mafuta kwenye vitalu namba 1 na 4 wamewakilishwa na kampuni ya Shell exploration and Production Tanzania Ltd.

Katika kitalu namba mbili iliwakilishwa na kampuni ya Equinor Tanzania AS.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!