July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atoboa siri machungu aliyopitia kufufua mradi wa gesi Mtwara

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema alipokuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alijaribu kutia mkono kwa lengo la kusukuma utekelezaji wa mradi wa uchakataji wa gesi asilia (LNG) lakini akashindwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema alichukua uamuzi huo kwani kwa muda wote ambao amekuwa akiitumikia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tangu akiwa waziri amekuwa akiusikia mradi huo wa LNG.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 11 Juni, 2022 Ikulu Chamwino jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya awali ya mkataba wa kuchakata gesi asilia.

“Kuna wakati nikiwa makamu wa rais nilijaribu kutia mkono na kuusukuma lakini tatizo lilikuwa zito na kulikuwa na mambo mengi ndani yake sikuweza.

“Nilipokabidhiwa nafasi hii ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nikaweka mguu chini nikasema hili lazima liwezekane,” amesema Rais Samia.

Aidha, amesema Aprili mwaka jana alitoa maelekezo kwamba zoezi la majadiliano kuhusu kufufua mradi huo lianze tena na kutoa miezi sita lakini bado ikakwama vilevile.

“Majadiliano hayakuanza kila nikiuliza najibiwa watalaam wanajipanga…Septemba nikabadilisha uongozi wa wizara ya nishati, nikaweka waziri mpya na nikamwambia sitaki tena kuona wataalam wanajipanga nataka timu mbili za serikali na wawekezaji zimeanza mazungumzo.

“Namshukuru Mungu, nashukuru timu zote, Januari Makamba na timu yako ya kusimamia na timu ya watalaam ambayo ilikuwa inapika issue za mazungumzo mpaka tumefikia leo kushuhudia zoezi la kusaini,” amesema Rais Samia.

Amesema anatambua makampuni yaliyokuwa yanatarajiwa kutekeleza mradi huo yalipata usumbufu wakati mwingine lakini sasa yameweka mguu chini kuanza majadiliano.

Amesema majadiliano ya awali yanatarajiwa kumazilika Disemba mwaka huu na kuanza awamu nyingine ya majadiliano kabla ya mradi kuanza kutekelezwa mwaka 2025.

Rais Samia amemshuhudia Waziri wa Nishati, Januari Makamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC), Dk. James Matarajio wakitia saini kwa upande wa Serikali na upande wa makampuni ya mafuta kwenye vitalu namba 1 na 4 wamewakilishwa na kampuni ya Shell exploration and Production Tanzania Ltd.

Katika kitalu namba mbili iliwakilishwa na kampuni ya Equinor Tanzania AS.

error: Content is protected !!