Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba yaachana na Pablo
MichezoTangulizi

Simba yaachana na Pablo

Aliyekuwa kocha wa Simba, Pablo Franco Martin
Spread the love

 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, klabu ya soka ya Simba imeachana rasmi na kocha wake Pablo Franco Martni mara baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Makubaliano hayo yamefikiwa hii leo tarehe 31 Mei 2022, huku klabu hiyo ikimtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya klabu hiyo.

Pablo alijiunga na Simba tarehe 10 Novemba 2022, Akichukua nafasi ya Didier Gomes, ambaye aliamua kuachana na timu hiyo kufutai matokeo mabaya aliyoyapata kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwenye msimu huu.

Aidha uongozi wa timu hiyo pia imevunja mkataba na kocha wake wa viungo Daniel De Castro Reyes Ambaye alijiunga na timu hiyo sambamba na Pablo.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo imeeleza kuwa, kwa sasa kikosi cha Simva kitakuwa chini ya mwalimu wao msaidizi Selamani Matola kwenye michezo mitano ya Ligi iliyosalia.

Pablo amevunjiwa mkataba wake siku chache, mara baada ya kupoteza pambano la nusu fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga lililofanyika jijini Mwanza, mara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Toka alipofika nchini Pablo amefanikiwa kuwapa Simba taji moja tu, la michuano ya kombe la Mapinduzi mara baada ya kuwafunga Azam FC kwenye fainali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!