Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa LIVE: Baraza Kuu Chadema, kina Mdee
Habari za SiasaTangulizi

LIVE: Baraza Kuu Chadema, kina Mdee

Spread the love

 

MKUTANO wa Baraza Kuu la chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema unafanyika leo Jumatano tarehe 11 Mei 2022, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Anayeongoza mkutano huo ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Pamoja na mambo mengine, baraza hilo litasikiliza rufaa za waliokuwa wanachama wao 19 akiwemo Halima Mdee ambap tarehe 27 Novemba 2020 walifukuzwa ndani ya chama hicho.

Walifukuzwa baada ya kutuhumiwa kqa usaliti, kughushi nyaraka za chama na kujipeleka bungeni kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum kinyume na taratibu za Chadema.

Kwa mujibu wa ratiba, agenda kuhusu rufaa hiyo ni ya mwisho kujadiliwa.

Mbali na Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine ni, waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Pia wamo, Hawa Mwaifunga, aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara); Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi na Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar na Katibu Mkuu, Bawacha-Bara, Jesca Kishoa

Wengine ni, aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo.

Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!