Spread the love

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limesaini mkataba na Kampuni ya ABSA yenye makao yake nchini Swiss utakaoliwezesha shirika hilo kuiuzia kampuni hiyo tani 60,000 za makaa ya mawe kila mwezi kwa  muda wa miaka mitano.  Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse akibadilishana Mkataba na Rais wa Kampuni ya ABSA, Bw.Gerges Schmickrath huku Naibu Waziri wa Madini, Dkt.Steven Kiruswa akishuhudia utiaji saini mkataba huo leo tarehe 10 Mei, 2022 jijini Dodoma.

Hafla hiyo ya utiaji saini mkataba huo imefanyika leo tarehe 10 Mei, 2022 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk. Venance Mwasse amesema, hatua hiyo ni matokeo ya jitihada na mikakati wa kuanza uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse na Rais wa Kampuni ya ABSA, Bw.Gerges Schmickrath wakionyesha Mktaba baada ya kusaini huku Naibu Waziri wa Madini, Dkt.Steven Kiruswa akishuhudia utiaji saini mkataba huo leo tarehe 10 Mei, 2022 jijini Dodoma.

Amesema thamani ya mkataba huo ni zaidi ya dola za Marekani milioni 108 sawa na Sh. bilioni 250 kwa miaka mitano

Aidha, Rais wa Kampuni ya ABSA, Gerges Schmickrath ameishukuru Wizara ya Madini kupitia STAMICO kwa kuaminiwa kuwekeza katika mradi huo wa makaa ya mawe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Drumlin Construction LTD ambaye ni msafirishaji wa makaa hayo nchini, Linus Seushy,akielezea jinsi alivyojiandaa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa kwakuwa ni jambo la kihistoria kwa nchi.

Amesema mradi huo utakuwa wa manufaa kwa Watanzania na kuongeza pato la Taifa. Makaa haya ya mawe yanayotoka mkoani Songwe katika mgodi wa Kabulo.

Naibu Waziri wa Madini, Dkt.Steven Kiruswa,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba mnono kati ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Kampuni ya ABSA ya nchini Uswiss leo tarehe 10 Mei, 2022 jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *