Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanajeshi 3,000 wa Ukraine wauawa
Kimataifa

Wanajeshi 3,000 wa Ukraine wauawa

Spread the love

 

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy amesema kati ya wanajeshi 2,500 na 3,000 wa Ukraine wamepoteza maisha hadi sasa katika vita kati ya taifa hilo na Urusi.

Aidha, amesema wanajeshi wengine kwamba 10,000 wamejeruhiwa.

Zelenskiy ametoa kauli hiyo jana tarehe 15 Aprili, 2022 wakati akizungumza na televisheni ya CNN ya Marekani katika kipindi hiki ambacho vita vya Urusi na Ukraine vikifikia siku 50.

Katika mahojiano hayo ambayo kwa upana yalirushwa mubashara Zelensky amesema wanajeshi wengine wa Ukraine takribani 10,000 wamejeruhiwa na ni vigumu kujua wangapi miongoni mwa hao watapona.

Zelensky amelinganisha idadi hiyo na ile ya Urusi inayoonesha wanajeshi wa Ukraine kati ya 19,000 na 20,000 wameuawa katika vita hivyo.

Mataifa ya Magharibi yanakadiriwa maelfu ya wanajeshi pia wameuawa kwa upande wa Urusi.

Lakini serikali ya Urusi hivi karibuni ilitangaza kuwa wanajeshi wake kiasi ya 1,350 wameuawa katika vita hivyo tangu vianze.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!