Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Papa Francisco amteua Padri Pisa Askofu Jimbo la Lindi
Habari Mchanganyiko

Papa Francisco amteua Padri Pisa Askofu Jimbo la Lindi

Padre Wolfgang Pisa
Spread the love

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisco, amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, Tawi la Arusha, Padre Wolfgang Pisa, kuwa Askofu wa Jimbo la Lindi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 9 Aprili 2022 na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Father Charles Kitima.

“Ubalozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania, unapenda kutaarifu kuwa, leo tarehe 9 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Francisco amemeteua Padri Wolfgang Pisa, Ofm, Capuchin, kuwa Askofu wa Jimbo la Lindi. Askofu mteule kwa sasa ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, tawi la arusha,” imesema taarifa ya Father Kitima.

Taarifa ya Father Kitima imesema, TEC inampongeza Askofu Mteule Wolfgang Pisa, kwa uteuzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Padri Richard A. Mjigwa, kutoka Vatican, Papa Francisco amemteua Padri Pisa kushika wadhifa huo, baada ya kuridhia ombi la Askofu Pius Ngonyani, la kung’atuka kwenye nafasi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!