Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, leo Jumapili tarehe 10 Aprili 2022, wanampokea Makamu Mwenyekiti wa chama hicho-Bara, Abdulraham Kinana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mapokezi hayo yanafanyika Ukumbi wa Diamond Jublee ambapo wanachama na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wamejitokeza kwa wingi na kuujaza.

Kinana anapokelewa Dar es Salaam baada ya kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu maalum tarehe 1 Aprili 2022 jijini Dodoma akichukua nafasi ya Philip Mangula aliyetangaza kung’atuka baada ya kukitumikia kwa kipindi kirefu.

Kinana amewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Fuatilia moja kwa moja kupitia MwanaHALISI TV

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *