Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kupanda bei mafuta: Wasira amkingia kifua Rais Samia
Habari za Siasa

Kupanda bei mafuta: Wasira amkingia kifua Rais Samia

Steven Wasira
Spread the love

 

MWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Mzee Stephen Wasira, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ana kazi ya kufanya katika kukabiliana na mfumuko wa bei ya mafuta katika soko la dunia, uliosababishwa na vita kati ya Urusi na Ukraine. Anaripoti Mwadishi Wetu, Pwani … (endelea).

Mzee Wasira ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, tarehe 9 Aprili 2022, akizungumza katika mdahalo wa kitaifa wa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyere, iliyofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.

Waziri huyo wa zamani wa Tanzania, amesema licha ya Rais Samia kuwa na sera ya maendeleo ya watu, bado ana kazi ya kufanya katika kukabiliana na athari ya vita hiyo iliyoibuka mwishoni mwa Februari 2022.

“Wakati Rais Samia anajitahidi sana kwenda na sera ya maendeleo ya watu, kwa sababu maendeleo lazima yawe ya watu, ndiyo maana mkazo wake uko katika mifumo inayozingatia maendeleo ya watu. Lakini bado ana kazi ya kufanya, kuna Ukraine na Urusi inapandisha bei ya mafuta,” amesema Mzee Wasira.

Mzee Wasira amesema “ukienda mtaani wanadhani Samia ndiye anaanzisha vita, kwa hiyo wanasema kwa nini bei hasimamii, Samia atasimamia bei lakini hawezi kuzuia kupanda kwa mafuta, sababu Urusi inayopigana ni ya tatu kutoa mafuta duniani ikishindwa kuuza sababu ya vikwazo kuna kuwa na upungufu wa mafuta na bei zinapanda.”

Mwanasiasa huyo amesema, wanaohoji kwa nini Rais Samia hasimamii mafuta , anamtwisha mzigo.

“Kukiwa na upungufu wa mafuta duniani bei zinapanda, ukisema Rais Samia kwa nini hasimamii mafuta, hii sasa unamwtisha mzigo,lakini naamini kila tunapoendelea kujifunza, tunajua nani ni nani na nini ni nini,” amesema Mzee Wasira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!