Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zungu amtoa hofu Rais Samia kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025
Habari za Siasa

Zungu amtoa hofu Rais Samia kuhusu Uchaguzi Mkuu 2025

Spread the love

NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu amemtaka Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, asiwe na hofu kuhusu Uchaguzi Mkuu ujao wa 2025, akisema wananchi wanampenda. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Zungu ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, tarehe 7 Machi 2022, akizungumza katika ziara ya Rais Samia kwenye Shule ya Sekondari ya Benjamini William Mkapa, jijini Dar es Salaam.

“Usiwe na hofu kuhusu uchaguzi unaokuja 2025, wananachi wote wanakupenda. Hawawezi kukupenda wote lakini wengi wanakupenda na wengi wamekubali na kwa dua za vijana hawa na dua za masheikh na wachungaji wetu mambo yatakwenda kuwa mazuri,” amesema Zungu.

Aidha, Zungu amesema Rais Samia amefanya jambo ambalo watangulizi wake, marais wastaafu, Hayati Benjamini William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete na Hayati John Pombe Magufuli, hawakulifanya, la kukutana na wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

“Kwa mujibu wa historia ya nchi yetu ni mara ya kwanza Rais ambaye yuko   katika madaraka anakutana na wanafunzi kama hawa leo, nilianza kazi zangu za siasa 2000, wakati Mzee Mkapa akiwa Rais hakufanya, JK hakufanya na hayati JPM hakufanya lakini wewe umefanya,” amesema Zungu.

Wakati huo huo, Zungu amemuomba Rais Samia aiboreshe Dar es Salaam, kwa kuiboreshea mazingira mazuri ya kiuchumi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu katika maeneo ya wafanyabiashara hasa Karikaoo na Upanga.

Aidha, amemuomba Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, asimamie mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP), awamu ya tatu, ili miundombinu ya jiji hilo ikamilike.

“Mkoa wa Dar es Salaam ndiyo unachangia mfuko mkuu wa Serikali kwa asilimia 75 mpaka 80, ukiliboresha Jiji la Dar es Salaam unaiboresha Tanzania , uchumi wa Dar es Salaam ukitetetereka nchi nayo inaweza kutetereka,” amesema Zungu na kuongeza:

“Nikuombe Rais maeneo ya Kariakoo, Upanga na maeneo yote ambayo kuna biashara, biashara nyingi zimepungua sababu miundombinu sio mizuri, lakini jitihada zinafanywa nakushuru sana.Waziri wa Fedha achangamkie fursa ya DMDP awamu ya tatu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!