Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanawake watakiwa kufanya kazi kwa bidii
Habari Mchanganyiko

Wanawake watakiwa kufanya kazi kwa bidii

Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sekunda Kasese
Spread the love

WANAWAKE katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wameshauriwa kufanya kazi kwa bidii na mshikamano ili kuhakikisha jiji hilo linasonga mbele katika nyanja zote za maendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo tarehe 6 Machi, 2022 Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Sekunda Kasese katika mahojiano maalum na Mwanahalisioline ofisini kwake mapema mwishoni mwa wiki.

Akizungumzia kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2022 isemayo “Kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu; tujitokeze kuhesabiwa” ameitaja kuwa ni muhimu.

Amesema kaulimbiu hiyo ni muhimu kushirikisha jinsia zote katika mipango ya maendeleo kuanzia ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla.

“Wanawake ni kundi kubwa katika jamii na wao wakishirikishwa katika mipango ya maendeleo, wanawake wanaweza na wanafanya vizuri. Hivyo, wakijitokeza kuhesabiwa kwa sababu ni sehemu kubwa ya jamii yetu wataiwezesha serikali kufikia malengo yake” alisema Mratibu Kasese.

Kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, alisema kuwa unafanya vizuri.

“Mpango wa kunusuru kaya masikini unafanya vizuri na unaendelea kufanya vizuri katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuinua hali ya umasikini wa jamii.

“Kundi kubwa la walengwa walio katika mpango wa kunusuru kaya masikini ni wanawake. Katika Jiji la Dodoma tuna jumla ya wanufaika 26,289, kati ya hao 16,101 ni wanawake walio katika rika mbalimbali na 10,188 ni wanaume.

“Wengi wanaopokea ruzuku ni wanawake tunajua mwanamke akipokea ruzuku ni fedha inayomsaidia yeye pamoja na kaya kwa ujumla sababu anapochukua fedha hiyo haipeleki katika mambo mengine yasiyofaa mfano ulevi wa kupindukia.

“Fedha anayopata anaipeleka kwenye biashara ndogondogo na shughuli nyingine za uzalishaji mali ili kuongeza kipato cha kaya” amesisitiza Kasese.

Mratibu huyo amesema kuwa wanawake wanufaika wa TASAF walio katika vikundi wanapata fursa ya mikopo ya wanawake ya asilimia nne kutoka mapato ya ndani inayotolewa na halmashauri ya jiji hilo.

“Ni ukweli usifichika kuwa mikopo inayotolewa na halmashauri kutoka mapato ya ndani imewanufaisha wanawake wengi tu wanufaika wa TASAF” amesema.

Amesema kuwa wanawake hao wamekuwa wakinufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia ‘community sessions’ ambazo wakufunzi mbalimbali hutoa elimu ya ujasiriamali, masuala ya lishe, ufugaji, utengenezaji sabuni na vyungu.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mwaka 2022 katika ngazi ya Mkoa wa Dodoma yatafanyika wilayani Chemba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!