Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Wazazi, walimu wapania kufuta ‘ziro’ Sekondari Makole
ElimuHabari Mchanganyiko

Wazazi, walimu wapania kufuta ‘ziro’ Sekondari Makole

Spread the love

WAZAZI na walezi wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Makole ambao wapo kidato cha pili na cha nne kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana na walimu kwa nia ya kuboresha elimu ya wanafunzi hao. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Wazazi walitoa maazimio hayo jana tarehe 5 Machi, 2022 wakati wa mkutano wa wazazi na walimu wa shule hiyo ulioitishwa na Mwenyekiti wa wazazi wa shule hiyo, Jonathani Jonas.

Akifungua mkutano huo Mwenyekiti huyo wa wazazi amesema lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya pande zote ili kupandisha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne ambao kwa pamoja wapo katika maadalizi ya mitihani ya Taifa.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na mtendaji wa kata, afisa elimu kata, afisa maendeleo kata pamoja na viongozi wa mtaa wa Ipagala, wazazi na walezi walisema jambo la kuboresha elimu ya mwanafunzi linaanza na mzazi mwenyewe kwa kushirikiana na walimu.

Awali, Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo, Revina Magomba alisema shule hiyo kwa miaka mitatu imepiga hatua ya ufaulu na lengo kubwa kwa sasa ni kuhakikisha wanafuta ziro.

Ufaulu wa kidato cha nne mwaka mwaka 2019 ulikuwa shule ya 27 ki-wilaya, 41 ki-mkoa kati ya shule 152, ya 1298 kitaifa kati ya shule 3908 na ufaulu kwa wastani wa asilimia 88.8.

Amesema ufaulu kidato cha nne mwaka 2020 ulikuwa 25 ki-wilaya kati ya shule 53, ki-mkoa 37 kati ya shule 168 na kitaifa ulikuwa ya 1254 kati ya shule 3956 sawa na asilimia 90.3.

Akizungumzia ufaulu wa kidato cha nne mwaka 2021 amesema shule hiyo ilikuwa ya 31 ki-wilaya kati ya shule 54, ki-mkoa ilikuwa ya 64 kati ya shule 187 na kitaifa ilikuwa ya 1587 kati ya 4141 sawa na asilimia 93.06.

Hata hivyo, mwalimu Migomba alisema kuwa kazi kubwa ni kuhakikisha wanafuta daraja ziro katika shule hiyo na kutafuta daraja la kwanza.

Aidha, amesema shule hiyo inakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo za watoto kukosa chakula pamoja na mashine ya kudurufu mitihani ya mazoezi.

Changamoto nyingine ni pamoja na wazazi kutokuwa na ushirikiano kati ya mzazi au mlezi mtoto na mwalimu jambo ambalo linasababisha mzazi kutokujua maendeleo ya mtoto na kutokuwa karibu na walimu.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Makole, Charles Shoidealiongeza kuwa shule hiyo haina uzio jambo linalosababisha wanafuzi kupata miaya ya kutoroka.

Aidha, baada ya kutokana kikao hicho, wazazi waliahidi kuimarisha ushirikiano na uongozi wa shule ili kupata taarifa za mara kwa mara juu ya maendeleo ya watoto wao.

Kwa upande wa wazazi Mussa Otyeno yeye alisema kwa nia njema wazazi wanakubaliana na hoja ya kushirikiana na walimu kwa lengo la kuboresha elimu ya watoto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!