Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari TFF yamfungia Shaffi Dauda miaka mitano
HabariMichezo

TFF yamfungia Shaffi Dauda miaka mitano

Spread the love

 

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania “TFF” limemfungia mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF Shaffi Dauda miaka mitano kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi pamoja na faini ya shilingi milioni sita hii leo 16 Feburuari 2022 jijini Dar es salaam. Anaripoti Ndelema Damas Tudarco ( endelea)

Taarifa hiyo iliyotolewa na TFF kupitia kurasa mbalimbali za mitandao yao ya kijamii imeeleza kuwa Shaffi Dauda alilalamikiwa kutoa taarifa za uongo na kuchochea umma kupitia mtandao wake wa instagram ambapo ni kinyume na kifungu cha 73(4)(a) na 75(5) vya kanuni za maadili ya TFF toleo la 2021 pia kwa kukiuka kifungu cha 3 (1) cha kanuni za utii za TFF toleo la 2021

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa kupitia kikao cha Kamati ya Maadili Ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania “TFF” kilichofanyika tarehe 14 na 15 februari 2022 ilisikiliza shauri hilo na akiwa mbele ya kamati mlalamikiwa Dauda alikiri kuchapisha taatifa hiyo lakini alidai akaunti yake inaendeshwa na watu wanne tofauti na wakati taarifa hiyo inachapishwa februari 8 2022 alikua safarini kutoka Cameroon kuja Dar es salaam hivyo hakupata nafasi ya kuihariri

Aidha kamati baada ya kumkuta na hatia katika makosa hayo imemfungia kujihusisha na shughuli za mpira ndani na nje ya nchi kwa miaka mitano na faini ya shillingi sita Millioni

Aidha TFF imemfungia mjumbe wa kamati ya utendaji ya Biashara United Hawaiju Gantala kifungo cha Maisha kujihusisha na soka baada ya kulalamikiwa na sekretatieti ya TFF kupeleka maswala ya mpira wa Miguu katika Mahakama za kawaida hivyo kushidwa kutii ibara ya 59(2) ya katiba la Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani “FIFA” ibala ya 66 ya katiba ya TFF toleo la 2019 na kifungu cha 6(1)(a) cha kanuni za maadili ya TFF toleo la 2021, mlalamikiwa alifungua kesi katika mahakama ya wilaya musoma kupinga uchaguzi wa klabu ya Biashara united

Hivyo kamati baada ya kumkuta na hatia ya kosa hilo imemfungia kujihusisha na soka maisha ndani na nje ya nchi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!