Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Zouma matatani kwa kumpiga paka teke ‘kama mpira’
HabariMichezo

Zouma matatani kwa kumpiga paka teke ‘kama mpira’

Spread the love

 

MCHEZAJI nyota wa Ligi Kuu ya Uingereza, Kurt Zouma anaweza kufunguliwa mashtaka baada ya kurekodiwa kwenye video akimpiga paka wake kama mpira kwenye sakafu ya jikoni yake.

Nyota huyo wa West Ham (27), pia ameonekana akimpiga kofi usoni paka huyo.

Klabu hiyo imelaani kitendo chake na kusema itashughulikia suala hilo ndani.

Beki huyo wa West Ham anaonekana akimshambulia mnyama huyo kwenye jumba lake la kifahari la pauni milioni 2 huku kaka yake akichukua video.

Zouma ameonekana akimdondosha paka huyo na kisha kumpiga teke hewani kwenye sakafu ya jikoni.

Zouma raia wa Ufaransa pia ameonekana akimfukuza mnyama huyo kuzunguka chumba chake cha kulia chakula mbele ya mtoto huku mpigapicha akicheka.

Katika clip ya mwisho, anaonekana akimpiga paka kwa nguvu usoni – na kutoka kwa mikono ya mtoto.

Jana usiku tarehe 8 Februari, 2022, Zouma ameomba radhi kwa shambulio hilo na kusisitiza kuwa lilikuwa tukio la pekee.

Amesema; “Naomba msamaha kwa vitendo vyangu. Hakuna visingizio kwa tabia yangu, ambayo ninajutia kwa dhati.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!