Saturday , 11 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kisa Shule ya Uongozi, Polepole atoa ujumbe
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kisa Shule ya Uongozi, Polepole atoa ujumbe

Humphrey Polepole
Spread the love

 

HUMPHREY Polepole, Mbunge wa Kuteuliwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa ujumbe kuzungumzia adhabu ya kusimamishwa kwa kipindi chake cha Shule ya Uongozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jana Ijumaa, tarehe 17 Desemba 2021, Kamati ya Maadili ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitagaza kukisimamisha kipindi hicho kwa muda mpaka pale kitakapopata wafanyakazi wenye uweledi.

TCRA ilisema, Polepole aliyewahi kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM na mjumbe wa iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba ana haki ya kukata rufaa ndani ya siku 21, kupitia Tume ya Ushindani (FCC).

Kipindi hicho, kilikuwa kinarushwa kupitia channel ya mtandaoni ya Polepole na kurasa zake zote za kijamii, akizungumzia masuala mbalimbali.

Baada ya uamuzi huo w TCRA, Polepole ameandika ujumbe na kuusambaza mitandaoni ukiwa na kichwa cha habari ‘Hatimaye hatima ya shule ya uongozi.

Ujumbe wote ni huu hapa;

Ufunuo 2:10b na Ahadi ya 8 ya Mwana CCM visomwe kwa pamoja.

Nimetafakari chapchap kwa kina sana. Nimegundua Utume wa Shule ya Uongozi umekamilika na umekamilika kwa Mafanikio Makubwa sana.

Kama zilivyokuwa amri 10 za Mungu kwa Bahati na mimi nilifanikiwa kufundisha na kutoa maarifa katika Episodi 10 ambapo nilijikita katika maeneo tofauti tofauti, kwa 10 hizi zilizosheheni Maarifa, inatosha!

Sitakata rufaa wala sitafanya maboresho katika Shule ya Uongozi kwasababu Utume ukikamilika, Umekamilika hakika!

Kwaheri Shule ya Uongozi, nimegundua sisi Viongozi tumetosheka kimaarifa, tunajua, tunafahamu na huwa hatupendezwi na Maarifa ya ziada.

Najua wananchi wa kawaida sana walifuatilia kwa wingi kutoka Mikoa yote na wengine nje ya Nchi.

Kwenu wafuatiliaji zaidi ya Milioni 5 wa kawaida Msifadhaike wala Msitahayari bado nina deni kubwa kwenu, nitaendelea kulilipa kwenu kivingine.

Msikate tamaa! Si wahenga walisema safari moja huanzisha nyingine ? Kuhusu kusema kweli, jambo moja nawaeleza hakika Aluta Continua!

NB: Kazi ya kufukiza moshi inaendelea

#kataawahuni

1 Comment

  • Asante ndugu pole pole miaka yote uliopangiwa kuishi duniani utakuwa ivyo ivyo huna hata moja lamana utakalo lifanya kazi yako ni fitina tu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

error: Content is protected !!