Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yapangua makatibu mikoa, wilaya
Habari za Siasa

CCM yapangua makatibu mikoa, wilaya

Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kujisuka upya kiuongozi baada ya kupanga-pangua makatibu wa mikoa na wilaya nchi nzima. Anaripoti Mwandishi Wetu,  Dodoma … (endelea).

Mabadiliko hayo ya makatibu wakuu ni kama yaliyofanyika hivi karibuni kwenye Jumuiya ya chama hicho kwa maana ile ya vijana (UVCCM), Wazee pamoja na wanawake (UWT) kwa kuwekwa wapya.

Mabadiliko hayo, yamekuwa yakifanyika ndani ya chama hicho, tangu kuingia madarakani kwa mwenyekiti mpya, Rais Samia Suluhu Hassan akipokea nafasi iliyoachwa wazi na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli.

Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021, baada ya Magufuli kufariki dunia siku mbili nyuma na baadaye mkutano mkuu wa CCM, iliokutana Dodoma ukamchagua kwa asilimia 100 Samia kuwa mwenyekiti.

Rais Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM

Taarifa ya Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, aliyoitoa leo Jumatatu, tarehe 8 Novemba 2021 imesema, kati ya makatibu 32 wa mikoa, 10 wamebaki vituo vyao vya kazi, waliopangiwa vituo vipya ni 12 na wapya ni tisa.

Shaka amesema, makatibu 168 wa wilaya ambapo waliopangiwa vituo vipya ni 67, waliobaki kwenye vituo vyao vya kazi ni 45 na wapya ni 56.

Amesema, katika kuzingatia suala la jinsia wanawake ni 67 sawa na asilimia 33.5, wanaume ni 133 sawa na asilimia 66.5.

“Katika uteuzi huu, hakuna hata mmoja aliyetoka nje ya mfumo wa Chama Cha Mapinduzi. Makatibu wapya wa mikoa na wilaya wametokana na kupandishwa hadhi kwa makatibu wa CCM wa wilaya, makatibu wa jumuiya za CCM wilaya na mikoa.

“Maafisa wa chama na jumuiya makao makuu kwa utendaji kazi wao mzuri pamoja na makatibu waliorejeshwa kwenye utumishi kutokana na utiifu wao kwa chama,” amesema Shaka

Katibu huyo wa uenezi alisema, uteuzi huo umeanza 6 Novemba 2021 na kamati kuu ya Halmashauri kuu iliyokutana jana Jumapili-Ikulu ya Dodoma ilizingatia sifa za ziada ikiwemo uadilifu, uaminifu, weledi, uwezo, bidii, ubunifu, jinsia na rika.

“Makatibu wapya na waliohamishwa vituo vya kazi kwa Mikoa na Wilaya wanatakiwa kuripoti vituo vyao vya kazi mara baada ya kupokea barua zao,” amesema Shaka

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!