Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Watanzania wanaoishi nje watumia trilioni 3.2, wanunua nyumba 135
Habari za Siasa

Watanzania wanaoishi nje watumia trilioni 3.2, wanunua nyumba 135

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo
Spread the love

 

SERIKALI imesema idadi ya Watanzania wapatao milioni 1.2 wanaoishi nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, wametuma nchini kupitia mifumo rasmi fedha za kigeni Dola za Marekani bilioni 2.3 sawa na Shilingi za Tanzania trilioni 5.3. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia imesema kwa upande wa sekta ya nyumba Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano wamenunua nyumba zaidi ya 135 zenye thamani ya Shilingi za Tanzania bilioni 29.7 kupitia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Hayo yameelezwa leo tarehe 8 Novemba, 2021 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.

Hamza alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Ritha Kabati (CCM), aliyehoji, Je, Serikali inayo database ya kutambua idadi ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi na nini mchango wa Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania katika kipindi cha miaka mitano?

Akijibu maswali hayo Hamza amesema Serikali imekuwa ikitumia mifumo mbalimbali ya kutambua Watanzania wanaoishi nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na usajili wao kupitia Balozi za Tanzania na Idara ya Uhamiaji kwa kutumia usajili wa hati za kusafiria za kielektroniki na hadi kufikia Januari, 2021 idadi ya Watanzania wapatao milioni 1.2  wanaishi nje ya nchi.

Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum Iringa (CCM)

Amesema Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

“Kwa mfano katika kipindi cha miaka mitano iliyopita mchango wao umehusisha sekta mbalimbali zikiwemo; sekta ya fedha, sekta ya afya na sekta ya nyumba. Kwa mfano, takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaonesha fedha za kigeni zilizotumwa (remittance) kupitia mifumo rasmi kutoka kwa Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ni takriban Dola za Marekani bilioni 2.3 sawa na Shilingi za Tanzania trilioni 5.3,” amesema.

Aidha, Amesema michango ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika Sekta ya Afya kwa kipindi cha miaka mitano inahusisha utoaji wa vifaa tiba, madawa, vitabu vya masuala mbalimbali ya afya na mafunzo ya elimu ya afya bora kwa wauguzi na madaktari kwenye hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa upande wa sekta ya nyumba amesema Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano wamenunua nyumba zaidi ya 135 zenye thamani ya Shilingi za Tanzania bilioni 29.7 kupitia Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

“Maelezo hayo hapo juu yanaonyesha ni kwa kiasi gani Watanzania wanaoishi nje ya Tanzania wanamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!