Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hati ya ukamatiji yaibu mvutano kesi ya Mbowe, yaahirishwa
Habari za SiasaTangulizi

Hati ya ukamatiji yaibu mvutano kesi ya Mbowe, yaahirishwa

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, imeahirisha usililizwaji wa kesi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake hadi kesho Jumanne, tarehe 9 Novemba 2021. Anariooti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni ili iandae uamuzi wa pingamizi la upande wa utetezi dhidi ya hati ya uchukuaji mali ya washtakiwa wawili katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kupanga njama za vitendo vya kigaidi.

Kesi hiyo imeahirishwa leo Jumatatu, tarehe 8 Novemba 2021 na mahakama hiyo mbele ya Jaji Joackim Tiganga, baada ya kuibuka mvutano kati ya mawakili wa jamhuri na utetezi kuhusu pingamizi hilo.

Hati hiyo inayopingwa ni ya uchukuaji mali za washtakiwa wawili, Adam Kasekwa na Mohammed Abdllah Ling’wenya, waliokamatwa maeneo ya Rau Madukani, Moshi mkoani Kilimanjaro, tarehe 5 Agosti 2020.

Ambayo ililetwa mahakamani hapo leo na Mkuu wa Upelelezi Wilayani Arumeru, Arusha, SP Jumanne Malangahe, akitoa ushahidi wake namna alivyowapekuwa washtakiwa hao, baada ya kukamatwa kwa kosa la kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi.

Jaji Tiganga ameahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo hadi kesho tarehe 9 Novemba 2021, atakapotoa uamuzi wa mahakama hiyo dhidi ya hati ya uchukuaji mali za washtakiwa hao, kama itapokelewa au haitapokelewa.

“Nikitazama muda sidhani kama nitaweza kamilisha uamuzi, naomba niahirishe mpaka kesho saa 3.00 asubuhi,” amesema Jaji Tiganga.

Mvutano huo wa kisheria uliibuka baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi hilo, ukidai hati hiyo limeletwa mahakamani hapo chini ya kifungu cha sheria ambacho hakipo.

Wakili wa utetezi, Nashon Nkungu, amedai kifungu cha 38 (3) cha Sura ya 20 ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, iliyofanyiwa marekebisho 2018, kilichotumika katika hati hiyo, hakipo katika sheria za nchi, kwa kuwa sheria hiyo haikufanyiwa marekebisho mwaka huo bali ilirekebishwa 2019.

Lakini upande wa jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, umepinga hoja hizo ukidai kwamba hazina mashiko kwa mujibu wa Sheria ya Kutafsiri Sheria.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

error: Content is protected !!