Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyewapekua wenzake Mbowe afunguka mahakamani
Habari za SiasaTangulizi

Aliyewapekua wenzake Mbowe afunguka mahakamani

Freeman Mbowe na wenzake wakiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

 

AFISA wa Polisi nchini Tanzania, Jumanne Malangahe, ametoa ushahidi wake katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyopo Mawasiliano jijini Dar es Salaam.

Shahidi huyo wa nane wa jamhuri, ameanza kutoa ushahidi wake leo Jumatatu, tarehe 8 Novemba 2021, mahakamani hapo mbele ya Jaji Joackim Tiganga, akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Halfan Hassan Bwire, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Shahidi huyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, ameileleza mahakama hiyo namna alivyowapekua washtakiwa wawili katika kesi hiyo, Kasekwa na Ling’wenya, walipokamatwa tarehe 5 Agosti 2020, maeneo ya Rau Madukani, mkoani Kilimanjaro.

Akiongozwa na Wakili Kidando, ASP Jumanne amedai, aliyekuwa Mkuu wa Upelele wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, ACP Ramadhan Kingai, alimuelekeza kuwafanyia upekuzi wa maungoni watuhumiwa hao baada ya kukamatwa wakituhumiwa kwa kosa la kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi.

Shahidi huyo wa Jamhuri alidai, baada ya kukabidhiwa majukumu hayo, aliwatafuta mashahidi huru waliokuwa karibu na kuwa alimpata Anita Mtali na Ester Ndunghulu.

Wakili Kidando: Baada ya kupata mashahidi ulifanyaje?

Shahidi: Baada ya mashahidi kutoka nilijitambulisha jina langu, niliwauliza majina watuhumiwa waliokuwa wamekaa chini wakajitambulisha.

Kabla ya kuwapekua, nilitoa mifuko ya suruali yangu kwamba sina chochote nao walishuhudia. Nikaagiza Kasekwa asimame, baada ya kusimama nilimwambia ageuke nyuma na anyooshe mikono juu.

Baada ya kumuamrisha hivyo alifanya, nilianza kumpapasa kichwani, sehenu ya kiwiliwili chake na sehemu ya kiunoni, nilihisi kitu kigumu upande wa kushoto nilipitisha mkono wangu na kuona hicho kitu kigumu ni bastola.

Wakili Kidando: Ilikuwa eneo gani ameiweka?

Shahidi: Ilikuwa kiunoni kwenye pindo la suruali.

Wakili Kidando: Ulifanya nini?

Shahidi: Nliichomoa silaha nikaonesha kwamba ni silaha, nikatoa magazini kulikuwa na risasi tatu, nikaonyesha wale mashaidii kisha nikampatia Detective Goodluck.

Nikaendelea kumpapasa zaidi maeneo ya kiunoni, baada ya kuingiza mkono wangu upande wa kushoto sikuona kitu, upande wa kulia nilipata simu ndogo aina ya Itel, kinaironi kilikuwa kimeviringishwa nikakinyoosha kilikuwa kimefungwa kama karanga, vilivyofungwa ilikuwa dawa za kuelvya baada ya kuzitoa nilianza kuzihesabu mbele ya mashahidi na watuhumiwa ikawa kete 58.

Wakili wa Serikali: Ulifanya nini kuhusiana na mtuhumiwa pili?

Shahidi: Nilimsimamisha nikamwambia ageuke nyuma, naye hivyo hivyo nilianza kumpekua kichwani hadi kiunoni sikuoana kitu.

Nikaingiza mkono mfukoni mwake upande wa kulia nilikuta simu kubwa aina ya Tecno, niliingiza zaidi mkono wangu nilikuta vikaratasi nikavihesabu mbele ya mashahidi na watuhumiwa ambavyo vilikuwa 25.

Nilivyomaliza mashahidi walisini fomu nikawapa nakala zake.

Wakili wa Serikali: Hati mbili za kuchukulia mali ulizikabidhi wapi?

Shahidi: Nilimoa Detective Goodluck, ambaye nilimoa vile vya mwanzo, akachukua fomu kusaini.

Wakili Kidando alimuuliza ASP Jumanne hizo mali zilizokamatwa anazitambuaje, amejibu akidai, bastola anaitambua kwa serial namba zake A5340, pamoja na jina lake la Ruger.

ASP Jumanne amedai, hati mbili za kuchukulia mali anazitambua kwa saini yake.

Wakili Kidando alimuuliza anaiomba nini mahakama, ASP Jumanne alijibu akidai anaiomba izipokee kama sehemu ya ushahidi wa Jamhuri.

Hata hivyo, upande wa utetezi umepinga nyaraka hiyo kwamba ziko kinyume cha sheria. Mvutano wa pande zote mbili unaendelea.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!