Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Majaliwa achangisha bilioni 1.6 za Taifa Stars
MichezoTangulizi

Majaliwa achangisha bilioni 1.6 za Taifa Stars

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania pamoja na wadau wa soka nchini kuungana kwa pamoja na kuhakikisha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa Miguu (Taifa Stars) inafanya vizuri kwenye michezo yote iliyobaki ili kufuzu kushiriki kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa wito huo jana Alhamis, tarehe 4 Novemba 2021, wakati akiongoza Kikao cha pamoja cha wadau wa soka Nchini katika ukumbi wa uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Ambapo katika kikao hicho wadau wa Taifa Star wamechangia Sh.1.6 Bilioni ambazo zitatumika kuihudumia timu katika maandalizi ya mechi zilizobaki za kufuzu kombe la Dunia.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Majaliwa amesema lengo la Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anakuza sekta ya michezo nchini na anataka kuona mafanikio katika timu za Taifa hivyo mikakati ya kuifanya timu ya Taifa ifanikiwe ni sehemu ya kutimiza malengo ya Rais.

Katika hatua nyingine Majaliwa ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda, Taasisi za Umma na binafsi pamoja na wadau wengine kuendelea kujitokeza kuichangia timu ya Taifa ili iweze kuweka Historia ya kushiriki kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Wadau Walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na GSM, TAIFA GAS, AZAM, CRDB, NBC, LAKE OIL, STAR OIL, K4 SECURITY, KAMBIASO pamoja na wadau wengine.

1 Comment

  • Hongera Waziri Mkuu Majaliwa,
    Naomba utumie pia usomi wako kufuatilia pesa hizo na mafunzo yawe ya hali ya juu na yasiwe legelege au babaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

error: Content is protected !!