Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi yawakamata wafuasi wa Chadema Kisutu
Habari za SiasaTangulizi

Polisi yawakamata wafuasi wa Chadema Kisutu

Wafuasi wa Chadema wakiwa chini ya ulinzi katika gari la polisi
Spread the love

 

BAADHI ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamekamatwa na Polisi Tanzania nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Wanachama hao wamekamatwa leo Alhamisi, tarehe 5 Agosti 2021, nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, walipofika kufuatilia kesi ya mwanyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake.

MwanaHALISI Online, limeshuhudia zaidi ya watu watano waliokamatwa ni miongoni mwa waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kupinga Mbowe kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi na kupanga njama za ugaidi.

Wanachama hao walikamatwa huku wengine wakifanikiwa kukimbia, baada ya kuinua mabango na kuimba nyimbo za kuhamasisha mwenyekiti wao aachwe huru kwa madai kwamba sio gaidi.

Baada ya wanachama hao kuanzisha nyimbo hizo, Polisi waliokuwa ndani ya magari wakiwa na silaha mbalimbali waliteremka na kuanza kuwakamata.

Kesi hiyo inayomkabili Mbowe na wenzake, ilikuwa inasikilizwa mahakamani hapo kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’, mbele ya Haki Mkazi Mkuu, Thomas Simba, lakini baadae iliahirishwa kutokana na tatizo la mtandao.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Halfani Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohammed Abdillahi Lingwenya.

Awali, washtakiwa hao walikuwa wanasikiliza kesi yao wakiwa katika mahabusu ya Ukonga, jijini Dar es Salaam, lakini ilishindwa kuendelea kutokana na tatizo la mtandao na kuahirishwa hadi kesho Ijumaa, saa 3:00 asubuhi.

 

Kufuatia changamoto hiyo, Hakimu Simba ametoa amri ya Mbowe na wenzake, wafikishwe mahakamani hapo kesho majira ya saa tatu asubuhi kwa ajili ya kuendelea na usikilizaji wa kesi hiyo.

Kwa mara ya kwanza Mbowe alipandishwa kizimbani tarehe 26 Julai 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi, mbele ya Hakimu Simba.

Katika mashtaka hayo, Mbowe anadaiwa kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi. Inadaiwa alitenda makosa hayo kati ya Mei na Agosti 2020, kwenye Hoteli ya Aishi, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!