May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtandao wakwamisha kesi ya Mbowe, Hakimu atoa maagizo

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imetoa amri ya kufikishwa mahakamani hapo kesho Ijumaa tarehe 6 Agosti 2021, saa 3:00 asubuhi, Freeman Mbowe na wenzake ili kufuatilia kesi inayowakabili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kupanga njama za ugaidi.

Kesi hiyo inayoendeshwa na Hakimu Mwandamizi, Thomas Simba, imeshindwa kuendelea leo Alhamisi, tarehe 5 Agosti 2021, baada ya mtandao kusumbua.

Mbowe na wenzake, walikuwa gereza la Ukonga wakifuatilia kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’ huku mawakili wa pande zote wakiwa chumba maalum cha Mahakama ya Kisutu.

Kesi hiyo ilikuwa imekwisha kuanza lakini kukatokea matatizo ya mtandao ambapo, upande mmoja ulikuwa hauoni picha ila unasikia sauti na mwingine unaona picha ila hausikii sauti jambo uliomfanya Hakimu Simba kuiahirisha.

Hakimu Simba amesema, ataandika ‘remove order’ ya kumtaka Mbowe na wenzake kufikishwa mahakamani hapo kesho Ijumaa na si vinginevyo.

error: Content is protected !!