Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Kisa ajali, michezo ya Ligi Kuu kusogezwa mbele
Michezo

Kisa ajali, michezo ya Ligi Kuu kusogezwa mbele

Kikosi cha timu ya Polisi Tanzania
Spread the love

 

KUFUATIA kupata ajali mbaya ya gari, kwa kikosi cha timu ya Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesogeza mbele kwa siku moja michezo ya mzunguko wa 33, kutoka Julai 14 mpaka Julai 15, 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikosi hiko cha timu ya Polisi Tanzania, kilipata ajali tarehe 9 Julai, 2021, walipokuwa wakitoka kwenye mazoezi kwenye Uwanja wa PTC, na kurejea kambini.

Katika ajali hiyo, mshambuliaji wa kikosi hiko, Mathias Mdamu aliumia vibaya kwa kuvunjika miguu yote miwili na kuendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya KCMC.

Afisa uhusiano Msaidizi wa Hospitali hiyo, Joel Masawe amesema kuwa maejeruhi walikuwa 13 na wanaendelea kupatiwa matibabu.

Gari la timu ya Polisi Tanzania lililopata ajali

“Mshambuliaji Mdamu ambaye alivunjika miguu yote, yeye yupo kwenye hali mbaya, lakini wachezaji wengine 13 wanaendelea kupatiwa matibabu,” alisema Afisa Habari huyo.

Taarifa kutoka bodi ya Ligi imeeleza kuwa, wameamua kuchukua hatua hiyo mara baada ya uongozi wa klabu hiyo kuomba kusogezea mbele mchezo wa wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.

Mzunguko huo wa 33 ulikuwa na michezo 11, ambayo ni Mbeya City dhidi ya Gwambina FC, Tanzania Prisons kuvaana na Biashara United, KMC kuwakabili JKT Tanzania, Yanga kuwaalika Ihefu, Dodoma Jiji dhidi ya Mtibwa Sugar, Coastal Union na Mwadui na mchezo wa mwisho ulikuwa Ruvu Shooting dhidi ya Namungo FC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!