Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sugu, Mchungaji Msigwa wawapeleka kortini AG, bosi magereza
Habari za SiasaTangulizi

Sugu, Mchungaji Msigwa wawapeleka kortini AG, bosi magereza

Spread the love

 

WABUNGE wa zamani wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania- Chadema, Mchungaji Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ wamewafungulia mashtaka Kamishna wa Magereza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) nchini humo kupinga adhabu zinazotolewa kwa wafugwa magerezani. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea)

Hayo yametolewa leo Jumatano, tarehe 2 Juni 2021, mkoani Dar es Salaam na wanasiasa hao wa upinzani, walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari.

Katika kesi hiyo, Sugu na Mchungaji Msigwa wanatetewa na mawakili wanne wakiwemo; Charles Tumain, Saimaon Patrick na Barnabas Kaniki.

Wakili Patrick amesema, kesi itasikilizwa tarehe 15 Juni 2021, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuanzia saa 8:00 mchana.

Kwa upande wake, Mchungaji Msigwa aliyeongoza Jimbo la Iringa kwa miaka kumi mfululizo kuanzia 2010-2020 amesema, Katiba ya Tanzania iliyoudwa mwaka 1977 inasema, binadamu huzaliwa huru na wote wana haki sawa, lakini wafugwa wengi hupitia mateso wanapokuwa gerezani.

“Watu wengi hawafahamu kwamba mtu anapokuwa gerezani anapitia mateso mengi kiasi gani, lakini ukweli ni kwamba mambo yanayotendeka kule, ni udhalilishaji na ni kinyume cha sheria na katiba yetu.”

“Adhabu zinazotolewa kule ni utaratibu ambao ulikuwa unatumika toka enzi za wakoloni, lakini mpaka sasa yanaendelezwa, jambo ambalo lishapitwa na wakati,” amesema Mchungaji Msigwa, aliyetuhumia adhabu gereza la Segerea, Dar es Salaam.

Naye Sugu aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini kwa miaka kumi kuanzia 2010-2020 amesema, lengo la kwenda kufungua mashtaka hayo mahakamani ni kwa ajili ya kuwatetea wafugwa.
Amesema, licha ya muda mrefu kupita tangu kumaliza kutumikiua adhabu zao, lakini wameona ni vyema kwenda mahakamani kutetea ukiukwaji wa haki za wafungwa wengine, wanaoendelea kutumikia adhabu zao.

Sugu na katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, walihukumiwa kifungo cha miezi mitano gerezani, kwenye gereza la Ruanda, Mkoani Mbeya Januari 2018.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!