Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Yanga, Morrison kuanza upya leo
Michezo

Yanga, Morrison kuanza upya leo

Spread the love

 

MAHAKAMA ya usuluhishi wa michezo kimataifa (CAS) imezitaka pande zote mbili kwenye kesi ya kimkataba kati ya Yanga na Morrison kutoa taarifa ya  kwanamna gani kesi hiyo itasikilizwa kwa kutumia nyaraka au kwa njia ya maneno kufikia leo tarehe 2 Juni, 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Hatua hiyo imekuja mara baada mahakama hiyo kutuma barua kwa uongozi wa Yanga juu ya mwenendo wa shauli hilo ambalo lilikuwa limesimama mara baada ya upande wa mchezaji Morison kuweka pingamizi la awali (Preliminary objection) kwa kutaka kesi hiyo kusikilizwa nchini.

Mara baada ya kuwasilisha leo mapendekezo ya namna gani kesi hiyo iendeshwe kwa pande zote mbili mahakama hiyo itaanza kusikiliza rasmi shauli hilo na kulitolea maamuzi.

Mwanasheria anaiwakilisha klabu ya yanga kwenye shauli hilo Alex Mgongolwa alinukuliwa kwenye chombo kimoja cha Habari akisema kuwa mara baada ya mlalamikiwa (Morrison) kupewa taarifa aliweka pingamizi la awali la kuwa mahakama ya CAS haina mamlaka ya kusikiliza kesi hile kwa kuwa klabu ya Yanga hawakuwa hawajamaliza hatua zote za ukataji rufaa zinazopatikana ndani ya nchi.

Makao Makuu ya Klabu ya Yanga

“Alivypewa taarifa mlalamikiwa ambaye ni Bernard Morrison alileta pingamizi la awali ya kwamba mahakama ya CAS haina mamlaka ya kusikiliza shauli lile kwa kuwa Yanga hawakumaliza hatua za ukataji rufaa ndani ya nchi kwa hiyo CAS wakatoa uamuzi ya kwamba wanamamlaka ya kusikiliza shauli lile na kama pingamizi lake lingekubalia inamaana rufaa ya Yanga ingeishia hapo.”Alisema Mgongolwa

Katika hatua nyingine Mgongolwa alisema kuwa mahakama hiyo iliwapa nafuu kwa pande zote mbili kwa kutaka kesi hiyo kusikilizwa kwa mdomo au kwa njia ya maandishi.

“Ni kweli walitupa nafuu siosi pande zote mbili kwa kwenda kuwakilisha kwa njia ya mdomo au maandishi kwa hiyo kwa sasa tunashauliana na wenzetu ni njia ipi sahihi ya kutumia.” Aliongezea Mgongolwa

Kwa upande wa klabu ya Yanga wao walitoa taarifa ya kuwa itaendelea kupambana kwenye shauli hilo mpaka haki itendeke.

Morrison aliingia kwenye mgogoro na klabu hiyo mara baada ya kujiunga na klabu ya Simba Agosti, 2020 huku klabu ya Yanga ikidai kuwa bado ilikuwa na mkataba na mchezaji huyo.

Kesi hiyo ilifika kwenye kamati ya Sheria na hadhi kwa wachezaji iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Elias Mwanjala ambao walitoa maamuzi ya kuwa mchezaji huyo yupo huru na halali kuichezea klabu ya Simba.

Mara baada ya hapo klabu ya Yanga haikulizika na hukumu hiyo na kuamua kukimbilia kwenye mahakama hiyo ya kimataifa ya michezo.

Morriso alifika nchini kwa mara ya kwanza tarehe 15 Januari, 2020 na kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miezi sita licha ya baadae klabu hiyo kudai kuwa mchezaji huyo aliongeza tena mkataba kwa miaka miwili.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!