May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kijiji Matinje kupelekewa mawasiliano

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inakusudia kutatua matatizo ya mawasiliano Kijiji cha Matinje Ikombandulu, ambalo ni eneo la machimbo lenye idadi kubwa ya watu ili kurahisisha biashara eneo hilo. Anaripoti Jemima Samwel DMC…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 2 Juni 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kundo Mathew katika kipindi cha maswali na majibu wakati akiwa anajibu swali la Seif Khamis Gulamali mbunge wa Manonga (CCM).

Mathew amesema, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote unatekeleza miradi mitatu katika Jimbo la Manonga.

“Miradi hiyo inatekelezwa katika Kata zaIgoweko(Mnara huu unahudumia pia Kata ya Uswaya), Sungwizi na Ngulu.Utekelezaji wa miradi katika kata hizi umekamilika.”

“Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itakifanyia tathmini Kijiji cha Matinje Ikombandulu na hatimaye kijiji hiki kitaingizwa katika orodha ya vijiji vitakavyojumuishwa katika zabuni zitakazotangazwa katika mwaka wa fedha 2021/22,” amesema Mathew.

error: Content is protected !!