Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania inavyotatua matatizo ya wakimbizi
Habari Mchanganyiko

Tanzania inavyotatua matatizo ya wakimbizi

Khamis Chilo, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema, jitihada zinaendelea kufanyika ili kumaliza tatizo la wakimbizi nchini humo kwa kuwarejesha makwao kwa kushirikiana na Jumuiya za Kimataifa na nchi wanazotoka. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Mara baada ya wakimbizi hao kuondoka, maeneo yote ya kambi za wakimbizi yatarejeshwa serikalini ili mamlaka zinazohusika ziweze kuyapangia matumizi stahiki.

Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 27 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Chilo wakatio akijibu swali la Agustine Holle, Mbunge wa Kasulu Vijijini (CCM).

“Kumekuwa na mgogoro wa ardhi wa muda mrefu baina ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na Kata ya Makere, je ni lini Serikali itatatua mgogoro huo,” ameuliza Holle

Akijibu swali hilo, naibu waziri wa wizara hiyo, Chilo amesema, kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu ilianzishwa mwaka 1996, kwa ajili ya kupokea wakimbizi kutoka nchi ya DRC.

Amesema, wakati wa uanzishwaji wa kambi hiyo, hakukuwa na mgogoro wa ardhi kwa sababu, lilikuwa eneo lisilotumika aidha pamoja na eneo la kambi, Serikali lilitenga eneo lingine la akiba kwa ajili ya wakimbizi iwapo eneo la awali litazidiwa.

“Kadri muda unavyokwenda, wananchi walianza kuvamia eneo la akiba kwa lengo la kuwatumia wakimbizi kama vibarua katika shughuli za kilimo katika eneo hilo.”

“Kwa kuzingatia maelezo hayo, ni wazi hakuna mgogoro wa ardhi baina ya kambi ya Nyarugusu na kata ya Makere, bali ni suala la uelewa ambapo wananchi wanaendelea kuelimishwa juu ya matumizi ya eneo hilo,” amesema Chilo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

error: Content is protected !!