Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Natamani kurudi nyumbani – Lema
Habari za SiasaTangulizi

Natamani kurudi nyumbani – Lema

Godbless Lema
Spread the love

 

GODBLESS Lema, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni Canada amesema, anatamani kurejea nyumbani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika moja ya Televisheni ya Mtandao, jana Jumatatu tarehe 19 Aprili 2020, Lema amesema atakapopata uthibitisho wa ulinzi wa maisha yake kutoka kwa mamlaka husika, atarejea nchini.

“Natamani kurudi nyumbani kushiriki sherehe za ndugu na rafiki zangu, lakini siwezi thubutu inaweza kuniletea maumivu makubwa, lakini mpaka pale nitakapopata uthibitisho wa uhakika kwamba, kuna haki na amani ya kutosha juu ya yangu.

“Experience (uzoefu) ngumu niliyonayo ya kwamba leo niko nje ya nyumbani nimeacha wazazi, rafiki na ndugu kwa kukimbia nchi. Ni experience mbaya sana, nisinge-wish (tamani) mwingine aipitie, hakuna experience mbaya kama umekimbia nyumbani halafu huji (hurudi) hata likizo,” amesema Lema.

Lemba ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini amesema, kwa sasa anamuomba Mungu ili Tanzania iendelee kuwa na amani na haki katika mihimili yake yote.

Godbless Lema, Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema)

“Nafuatilia nyumbani kuliko mtu yoyote na naombea nyumbani kuliko mtu yoyote, kama kuna mtu pengine anayefanya sala kuona nyumbani pana badilika haraka na kuwa na amani na haki, kuanzia mahakama, polisi, bunge na serikali ni mimi,” amesema Lema.

Mwanasiasa huyo pamoja na familia yake, waliondoka nchini Tanzania Novemba 2020, kwa madai ya kupata vitisho vya usalama wake, baada ya uchaguzi mkuu.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, Lema aligombea Ubunge Arusha Mjini kupitia Chadema, na kuangushwa na Mrisho Gambo, aliyetangazwa mshindi wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lema aliungana na Lissu, aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema katika uchaguzi huo,kuondoka nchini Tanzania kwa madai ya kuhofia usalama wa maisha yao.

Hata hivyo, zaidi ya mara mbili Insepekta Jenerali wa Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro aliwaita wanasiasa wote waliokimbia nchi warudi nchini, huku akiwahakikishia ulinzi.

1 Comment

  • Asante ndugu lema uhakika wa usalama kwa watu wote wanaishi tanzania upo na niwauakika .lema umekukimbiza aibu yako mwenye ulijtangazi ubunge wa kudumu kumbe ulikuwa unadaganya na kujidanya kwa kuona aibu umeona bora uwende ktk bara ambalo mtu mweusi anadharauliwa na kunyanyaswa kwa rangi yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!