JESHI la Polisi Tanzania, limeeleza kwamba lilimkamata mwigizaji Kajala na mwanaye Paulina kwa tuhuma za kusambaza picha za utupu za msanii wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema, wawili hao walikamatwa jana muda mfupi baada ya kutua katika ardhi ya Tanzania wakitokea Dubai.
Hata hivyo amesema, baada ya mahojiano na wawili hao, waliachwa kwa dhamana.

“Tuliwakamata na tukawahoji baada ya mlalamikaji (Harmonize) kuleta malalamiko kituoni, hata hivyo tayari tumewaachia kwa dhamana,” amesema Kamanda Mambosasa.
Pamoja na kuachwa kwa dhamana, Kamanda Mambosasa amesema, wawili hao wataendelea kuripoti kituo cha polisi mpaka pale uchunguzi utakapokamilika na kisha kupelekwa mahamani.
Leave a comment