Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba yaweka rekodi dhidi ya kocha wa Al Ahly
MichezoTangulizi

Simba yaweka rekodi dhidi ya kocha wa Al Ahly

Spread the love

 

USHINDI wa bao 1-0, dhidi ya Al Ahly walioupata Simba kwenye uwanja wa Mkapa, mchezo wa kundi A wa Ligu ya Mabingwa Afrika, umewafanya kuwa timu ya kwanza ndani ya Afrika kumfunga, Pitso Mosimane toka alipoaanza kukinoa kikosi hiko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Pitso ambaye ni raia wa Afrika Kusini alijiunga na miamba hiyo ya soka nchini Misri akitokea Mamelodi Sundown mwezi Septemba 2020.

Tarehe 30 Septemba 2020, klabu ya Al Ahly ilimtambulisha Pitso kama kocha wao mpya na kuingoza timu hiyo kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwafunga Zamalek.

Kocha huyo toka alipoichukua Al Ahly ameiongoza kwenye michezo saba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika michezo hiyo saba kocha huyo alifanikiwa kushinda michezo sita na leo dhidi ya Simba ulikuwa mchezo wa saba na kukubali kichapo kwa mara ya kwanza.

Pitso alianza kibarua chake ndani ya Al Ahly dhidi ya Raja Athletic Club katika mchezo wa nusu fainali na kushinda mechi zote mbili na baadaye kuivaa Zamalek na kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa fainali katika msimu uliopita.

Kuanza kwa msimu huu wa 2020/21, Pitso ameiongoza Al Ahly katika michezo mitano, miwili kati ya hiyo ni alishinda kwenye hatua ya awali na baadae kwenda El Merreikh kwenye mchezo wa hatua ya makundi.

Bao la Simba lilifungwa na Luis Miquison dakika ya 31, na kuifanya timu hiyo kuondoka kifua mbele kwa pointi tatu na kukaa kileleni kwenye kundi A.

Hii ni mara ya pili kwa Al Ahly kufungwa kwenye ardhi ya Tanzania na Simba kama ilivyotokea 2019, walipopoteza kwa bao 1-0, kwenye Uwanja wa Mkapa bao lililofungwa na Meddie Kagere.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!