May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaifanyia mbaya Al Ahly

Spread the love

 

BAO pekee la Luiz Miquison lilitosha kuiangamiza Al Ahly kwenye mchezo wa kombe la Ligu ya Mabingwa Afrika, katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dares Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa kundi A, ulianza majira ya saa 10 jioni ambao kila timu ilikuwa inacheza kwa tahadhari kubwa kutokana na ubora wa timu zote mbili.

Kipindi cha kwanza Simba walionekana kushambulia sana lango la Al Ahly na kufanikiwa kuandika bao dakika ya 31 kupitia kwa Miquison na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Simba wakiwa mbele kwa bao 1.

Kipindi cha pili kilianza kwa taratibu kwa timu zote mbili, lakini Simba walionekana kumiliki mpira kwa asilimia kubwa baada ya kufanya mabadiliko kwa kumtoa Hassan Dilunga na kuingia Larry Bwalya.

Mpaka dakika 90 zinakamilika Simba kufanikiwa kuibuka na pointi tatu zinazowasogeza kwenye kilele cha kundi hilo wakiwa na pointi sita baada ya kushinda michezo yao miwili.

Mchezo unaofuata Simba atafunga safari kwenda nchini Sudan kuvaana na El Merreikh ambao leo wamepoteza mchezo wao dhidi ya AS Vita Club kwa mabao 4-1.

error: Content is protected !!