Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Uamuzi wa CAF waibeba Namungo FC
Michezo

Uamuzi wa CAF waibeba Namungo FC

Kikosi cha Namungo
Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), limeamua michezo yote miwili ya Kombe la Shirikisho kati ya Namungo FC na CD 1 Agosto ya Angola kuchezwa hapa nchini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam…(endelea).

Ni baada ya kamati ya mashindano ya CAF kubaini kuwa, katika timu hizo hakuna iliyokwamisha kuchezwa kwa mechi yao ya kwanza.

Mchezo wa kwanza wa michuano hiyo, ulipangwa kuchezwa nchini Angola tarehe 14 Februari 2021.

Hata hivyo, haukuchezwa kutokana na maofisa wa serikali nchini Angola kuitaka Namungo kukaa karantini au kurejea Tanzania mara baada ya wachezaji wao watatu pamoja na kiongozi mmoja kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Katika taarifa yao CAF iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeleeza mara baada ya kufutwa kwa mchezo huo hapo awali, CAF kupitia kamati ya mashindano, imeamua michezo hiyo ipigwe hapa nchini ndani ya saa 72 mpaka kufikia tarehe 26 Februari 2021.

Baadhi ya wachezaji wa CD 1 Agosto

Kwenye michezo hiyo, CD 1 Agosto itahesabika kuwa mwenyeji katika mechi yake wa kwanza na hivyo kubeba ghalama zote za mchezo huo, ikiwemo waamuzi.

Kisha Namungo FC watakuwa wanyeji kwenye mchezo wa pili utakaochezwa ndani ya saa 72, toka mchezo wa kwanza utakapo fanyika.

Aidha CAF imeeleza kuwa, timu yoyote itakayopita kwenye mchezo huo, haitazingatiwa viwango kwenye upangawji wa hatua ya makundi wa michuano hiyo ya kombe la shirikisho, katika droo itakayo fanyika tarehe 22 Februari 2021.

Ikumbukwe mchezo huu ni wa mzunguko wa tatu wa michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mshindi kwenye mchezo huu, ataingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!