May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BREAKING NEWS: Maalim Seif afariki dunia

Spread the love

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ametangaza kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad (77), Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar, kilichotolea leo Jumatano saa 5:00 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Rais Mwinyi amesema, Maalim Seif aliyezaliwa tarehe 22 Oktoba 1943 visiwani Pemba, alikuwa akipatiwa matibabu Hospitali ya Muhimbili tangu 9 Februari 2021.

Rais Mwinyi ametangaza siku saba za maombolezo, yatakayoambatana na bendera kupepea nusu mlingoti huku taratibu za mazishi zitatangazwa baadaye kwa ushirikiano na chama chake cha ACT-Wazalendo.

Hadi anafikwa na mauti, Maalim Seif alikuwa Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

error: Content is protected !!