Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Ethiopia apimwa joto, ‘apakwa’ vitakasa mikono Chato
Habari za SiasaTangulizi

Rais Ethiopia apimwa joto, ‘apakwa’ vitakasa mikono Chato

Spread the love

 

KATIKA kuchukua tahadhari dhidi ya kusambaa kwa maambukizo ya virusi vya corona (COVID-19), Sahle – Work Zewde, Rais wa Ethiopia amepimwa joto na kupaka vilainishi kabla ya kukutana na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Work Zewde ametua Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Geita uliopo wilayani Chato leo Jumatatu tarehe 25 Januari 2021, katika ziara ya kikazi ya siku moja.

Rais huyo ameongozana na maofisa mbalimbali kutoka nchini mwake.

Baada ya kufunguliwa kwa mlango wa ndege aliyosafiria, Work Zewde alishuka huku akiongozana na maofisa wake (mmoja mwanamama na mwingine mwanaume), wote wakiwa wamevaa barakoa.

Wakati akishuka, gwaride lilikuwa likiendelea huku Rais Magufuli akiwa mbali kidogo na mwisho wa gazi za ndege hiyo.

Baada ya kukanyaka ardhi ya Tanzania, Work Zewde na wenzake walikutana na ofisa wa Tanzania akamiminiwa kimiminika (sanitizer), naye alikipaka kwenye mikono yake.

Baada ya zoezi hilo, alisogea kwa ofisa wa pili aliyekuwa karibu na aliyempatia kitakasa mikono kisha kifaa akampima joto. Hatua hizo zilipitiwa na maofisa wote alioambatana nao.

Lakini ofisa wa Tanzania aliyempima joto Rais Work Zewde na yule aliyempatia kimiminika, wote hawakuvaa barakoa wala chochote kwenye mikono yao.

Rais huyo kisha alisogea pale aliposimama Rais Magufuli, walisalimiana bila kushikana mikono. Rais Magufuli, waandishi wa habari na maofisa wengine pia hawakuwa wamevaa barakoa.

Rais Magufuli alianza kumkaribisha mgeni wake kwa lugha ya kiingereza ‘good morning’ kwa maana ya habari za asubuhi, mgeni huyo aliitikia ‘fine’ kwa maana ya salama.

Kisha Rais Magufuli alimkaribsha kwa lugha ya Kiswahili, ‘karibu sana.’

Baada ya ukaribisho huo, Rais Magufuli na mgeni wake walipita katikati ya wanajeshi walioshikilia mitutu moja kwa moja kwenda kusalimiana na maofisa wengine wa Tanzania na kuangalia burudani ya za ngoma zilizokuwapo uwanjani hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!