May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kuanza mazoezi leo

Hassan Bumbuli, Afisa Habari wa Yanga

Spread the love

 

BAADA ya mapumziko ya siku 10, hatimaye kikosi cha Yanga kitaanza mazoezi leo kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mzunguko wa pili itakayoanza tarehe 13 Februari 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Ligi hiyo ambayo imesimama kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na ile ya mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), itaendelea kuanzia tarehe 4 Februari kwa timu zilizokuwa na michezo mkononi.

Afisa Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa tayari wachezaji wameshaanza kuwasili kambini isaipokuwa Fistoni Abdul Razak ambaye wanatarajia kati ya leo jioni au kesho watakuwa nae.

“Wachezaji wameanza kuripoti kambini ikiwemo nahodha Lamine Moro ambaye amesharejea nchini akitokea Ghana na mara baada ya kurudi alimpigia simu meneja wa timu na kumueleza kwamba ameshafika hivyo anaonesha mfano mzuri kwa wenzake akiwa kama kiongozi.

“Fiston Abdul Aziz ambaye ni mchezaji wetu mpya tunatarajia kati ya leo jioni au kesho tutakuwa nae, amechelewa kutokana na ruti nyingi za ndege kufa” alisema Bumbuli

Pia Afisa Habari huyo aliongelea kuhusu wachezaji waliokuwa majeruhi kwenye kikosi hiko, kwamba wote wataripoti kambini kutokana na kuendelea vizuri isipokuwa mchzaji Mapinduzi Balama ambaye bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari.

error: Content is protected !!