Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Wachezaji watatu, timu ya Taifa Congo wakutwa na Corona
Michezo

Wachezaji watatu, timu ya Taifa Congo wakutwa na Corona

Spread the love

 

KUELEKEA mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wandani (CHAN), wachezaji watatu wa timu ya Taifa ya Congo DR akiwemo mlinda mlango wao Nathan Mabruki wamekutwa na Corona na hivyo kuukosa mchezo wa leo dhidi ya Niger. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Wachezaji wengine ni William Luezi na Ricky Tulengi ambao wote kwa pamoja wamekutwa na maambukizi hayo mara baada ya kuchukuliwa vipimo saa chache kabla ya mchezo kama ilivyo kwenye kanuni za michuano hiyo.

Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hiyo kukosa huduma ya baadhi ya nyota wake kutokana na kukutwa na virusi vya Corona, kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza ambapo wachezaji wao watano walikaa nje kutokana na kukutwa na maambukizi hayo licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bahati mbaya haikuishia hapo tu, kwenye mchezo wa pili wa kundi hilo dhidi ya Libya ambao walitoka sare ya bao 1-1, Congo DR walikosa huduma ya kocha wake, Florent Ibenge ambaye alikutwa na maambuki hayo.

Congo DR ambao ni vinara wa kundi B, baada ya kuwa na pointi nne, itacheza mchezo wake wa mwisho hii leo kwenye hatua hiyo dhidi ya Niger ambayo inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi mbili, huku kila timu ikiitaji ushindi wa aina yoyote kuweza kufuzu kwenye hatua inayofuata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!