Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko RC aeleza machungu ya polisi kwa raia
Habari Mchanganyiko

RC aeleza machungu ya polisi kwa raia

Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Spread the love

 

ANTHONY Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC), amelalamikia hatua ya haki za raia kuanza kutoweka katika mikono ya Jeshi la Polisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu … (endelea).

Amesema, kutokana na kutoweka kwa haki hizo, watu wengi wamekuwa wakifungwa bila kuwa na hatia na kwamba, amelitaka jeshi hilo kubadili tabia.

“Msingi wa haki na utu uanzie kwenye Jeshi la Polisi, hawa ndiyo wahusika wa awali kabisa kwenye kesi yoyote, kama hivyo vitu havitakuwapo, ni ngumu myonge kupata haki hivyo,” amesema.

Akizungumza jana Jumapili tarehe 24 Januari 2021, kwenye uzinduzi wa Wiki ya Sheria na Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mahakama, Bariadi mkoani Simiyu.

“Jeshi la Polisi libadilike katika utendaji kazi kwa kuwa, haki ya mtuhumiwa huanza kupotea kwenye eneo lao kabla ya kufikishwa mahakamani na kusababisha watu wengi kufungwe bila hatia,” amesema.

Amesema, kumekuwepo na kiwango kikubwa cha malalamiko ya raia kubambikiziwa kesi na kusababisha, wengine kujikuta wakifungwa.

Amesema, iwapo mkamataji na mpelelezi wataamua kusema uongo, raia huyo hawezi kupata haki na matokeo yake ataingizwa kwenye matatizo.

“Endapo mkamataji na mpelelezi watasema uongo, hakuna haki hata kidogo hapo na hakimu au mahakama inaweza kushindwa kupata ukweli ikaonekana uongo wa polisi ndiyo ukweli,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!