Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Taasisi 20 za Serikali zapewa siku 30 kulipa bilioni 30 za TTCL
Habari za Siasa

Taasisi 20 za Serikali zapewa siku 30 kulipa bilioni 30 za TTCL

Spread the love

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile amezipa siku 30 taasisi za umma zinazodaiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kulipa madeni wanayodaiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, lengo ni shirika hilo liweze kujiendesha, kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma ya mawasiliano ya sauti na data kwa taasisi za Serikali, sekta binafsi na wananchi ili kukuza uchumi na kuchangia pato la taifa.

Dk. Ndugulile ameyasema hayo wakati wa ziara yake alipotembelea TTCL kwa lengo la kufahamiana na kuzungumza na wajumbe wa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wa TTCL, Dar es Salaam ambapo aliambatana na naibu waziri wake, Mhandisi Kundo Mathew na Mejimenti ya wizara hiyo.

Amesena, zaidi ya taasisi 20 za Serikali zinadaiwa na TTCL zaidi ya Sh. 30 bilioni ambapo zipo taasisi zinatumia huduma za mawasiliano za TTCL na zinakusanya mapato ya zaidi ya Sh.1 bilioni kwa mwezi ila hawako tayari kulipa huduma za TTCL.

Vile vile, ametoa onyo kali kwa kampuni zinazohujumu miundombinu ya TTCL ili ishindwe kutoa huduma za mawasiliano kwa wateja wake kuwa waache tabia hiyo mara moja na wafanye biashara kwa misingi ya ushindani, vinginevyo Serikali itawachukulia hatua kali.

Aidha, amesisitiza kwa watakaoiba nyaya za shaba za TTCL na kuuza kama chuma chakavu nao waache mara moja kwa kuwa watahusishwa na uhujumu uchumi kwa kudhoofisha utendaji kazi wa TTCL na kwa watakaobainika watachukuliwa hatua kali na Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Amewataka watendaji wa Wizara kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kufanya utafiti na tathmini ya kubaini mchango wa sekta hii aidha wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja katika kukuza uchumi na kuchangia pato la taifa.

Naye Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew amewataka watumishi wa TTCL kuwa wabunifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na wajenge utaratibu wa kufuata na kuwahudumia wateja huko waliko badala ya kusubiri wateja kuwafuata ofisini.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema, amepokea maelekezo ya Dk. Ndugulile na ametoa rai kwa watumishi wote wa TTCL kujituma ili kuongeza upatikanaji wa huduma ya mawasiliano yenye kasi ya brodibandi kutoka asilimia 49 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 80 mwaka 2025.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!