Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waliomuua Mawazo wa Chadema, nao kunyongwa
Habari Mchanganyiko

Waliomuua Mawazo wa Chadema, nao kunyongwa

Kitanzi
Spread the love
MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Mwanza, imewahukumu kunyongwa hadi kufa, kwa  washitakiwa wanne waliotuhumiwa na Jamhuri, kumuua kwa makusudi,  Alphonce Mawazo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Waliopatikana na hatia ya kumua Mawazo, ambaye alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Geita, ni pamoja na aliyekuwa mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiy, Alfan Apolnar.

Wengine walioadhibiwa kunyongwa hadi kufa, ni mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo, Epafra Zakaria, mshitakiwa wa tatu, Hashim Sharif na aliyekuwa mshitakiwa wa tano, Kalulinda Bwire.

Wote kwa pamoja walidaiwa kumuua kada huyo wa Chadema ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Ziwa, tarehe 14 Novemba mwaka 2015.

 

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani, washitakiwa wote hao, pamoja na kukana madai hayo mahakamani, lakini walitajwa na mashahidi karibu wote wa Jamhuri kuhusika na mauaji hayo.

Mawazo aliuawa siku chache baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Katika uchaguzi huo Mawazo aligombea ubunge jimbo la Busanda.

Katika shauri hilo namba tisa la mwaka 2019, mshatakiwa wa nne, Habibu Feruzi ameachiwa huru baada ya ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kushindwa kuthibitisha kuhusika kwake kwenye mauaji hayo ya kukusudia.

Hakimu mwandamizi mwenye mamlaka ya juu kusikiliza kesi ya mauaji, Frank Mahimbali, ameieleza mahakama kuwa baada ya kuitafakari kesi yote na kusikiliza upande wa mashtaka na mashahidi 13 pamoja na vielelezo vitano na ushahidi, mahakama imewakuta na hatia washtakiwa wanne.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!