Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Bagonza: Amani hailetwi kwa majeshi
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Bagonza: Amani hailetwi kwa majeshi

Askofu Benson Kagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe
Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT), Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera, Dk. Benson Bagonza, amani hailetwi kwa majeshi, itikadi yoyote au fadhila za wafalme wa dunia, bali huletwa na ujio wa Mungu katika maisha yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Amewaomba Wakristo na Watanzania kuadhimisha Sikuu ya Noel (Christmas) na mwaka mpya, kwa kuienzi tunu ya amani.

Wito huo alioutoa tarehe 3 Desemba 2020 na kuanza kusambazwa jana tarehe 23 Desemba 2020, umebeba ujumbe kutoka Kitabu cha Isaya sura ya 9:6 inayosema “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, mshauri wa ajabu, mfalme wa amani.”

“Kwa mara nyingine Nabii Isaya anatukumbusha asili ya amani tuliyo nayo, kwamba haikuletwa na majeshi, vifaa vya kisasa, itikadi yoyote, ujanja wa wanadamu na fadhila za wafalme wa dunia. Amani ya kweli kiblibilia ni tunda la ujio wa Mungu katika maisha yetu,” ameandika Askofu Bagonza.

Amesema, amani isiyotokana na Mungu ni ya muda na kwamba, hushindwa kudumu muda mrefu.

“Kwa ajili yetu sote Mungu alifanya mwili, akazaliwa kama sisi, katika sifa nyingi alizo nazo, yeye ni mfalme wa amani, amani za bandia zilishindwa, Mungu akaja mwenyewe,” amesema Askofu Bagonza.

Kiongozi huyo wa kiroho ametoa wito huo katika salamu zake za Sikuu ya Christmas na mwaka mpya, kwa waumini KKKT, Dayosisi ya Karagwe na Watanzania kwa ujumla.

Amesema “amani isiyotokana na mfalme huyu (Yesu Kristo) ni ya muda tu, ni utulivu uliojaa ukimya, ni uvumilivu usio na upendo, ni woga kwa mwanadamu na utii kwa sanamu. Ni ustaarabu uliojaa ubinafsi.”

Askofu Bagonza amesema, amani inayoletwa na Yesu Kristo imejengwa juu ya haki ambayo inakataa kila aina ya dhuluma.

“Amani aletayo Yesu Kristo imejengwa juu ya haki, upendo, kujali wengine, kutetea walio dhaifu na kukataa kila aina ya dhuluma.  Yesu ni mfalme  wa amani kwa sababu hakuuwa bali aliuawa, hakutukana bali alitukanwa, hakubagua watu bali alibaguliwa.

“Alisifiwa lakini alikataa kusifiwa, hakuonea bali alionewa. Hakubambikia mtu kesi, bali alibambikiwa kesi na mwisho hakutumbua mtu yoyote bali alitumbuliwa na kunyang’anywa ufalme wake kama jambazi msalabani. Kazi yake na mafudisho yake vililenga kutumbua dhambi na kutangaza haki iletayo amani,” amesema Askofu Bagonza.

Katika salamu hizo, Askofu Bagonza amewaomba Wakristo wote wampokee Yesu katika maisha yao kwa sababu kwake yeye, wanyonge na wenye nguvu wana nafasi sawa ya kukombolewa.

“Tunaalikwa kumpokea mtoto Yesu katika maisha yetu, yeye anayo amani ya kweli kwa ajili yetu. Aliuacha U-Mungu wake, akashirikiana na wenye dhambi pamoja na wote waliobaguliwa, anatuita sote wenye mizigo na kulemewa na dhambi twende kwake,” amesema Askofu Bagonza na kuongeza.

“ Mbele yake wanyonge na wenye nguvu wana nafasi sawa ya kukombolewa, anayo kiu ya haki kwa ajili ya ulimwengu wote.  Wote waliompokea aliwaafanya kuwa wana wa Mungu, nawatakiwa Noeli yenye baraka na mwaka mpya wa amani ya kweli.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!