Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Aliyeshindwa kuapa, aombewa kazi kwa JPM
Habari za SiasaTangulizi

Aliyeshindwa kuapa, aombewa kazi kwa JPM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania kumwombea Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mkoa wa Lindi, Francis Ndulane aliyeshindwa kuapa kuwa Naibu Waziri wa Madini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pia, Majaliwa amemwomba Rais John Pombe Magufuli kuangalia nafasi zingine ili kumpa tena Ndulane.

Majaliwa ametoa ombi hilo leo Ijumaa tarehe tarehe 11 Desemba 2020 muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kumaliza kumwapisha Profesa Shukrani Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Profesa Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, ameteuliwa leo Ijumaa asubuhi kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais na naibu waziri wa madini.

Spika Job Ndugai, alimwapisha Profesa Manya kuwa mbunge leo asubuhi viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Ndulane alikutwa na kadhia ya kushindwa kuapa tarehe 9 Desemba 2020 na kujikuta akisoma kiapo kwa kuweweseka jambo lililomfanya Rais Magufuli kueleza atafanya uteuzi upya wa naibu waziri wa madini.

Mara baada kumaliza kuapishwa na Rais Magufuli, salamu mbalimbali zimetolewa ambapo, Majaliwa na Spika Ndugai wamejikuta wakizungumzia sakata hilo ambalo baada ya kushindwa kuapa, liliibua mjadala.

Spika Ndugai amesema, “tunakupongeza sana kwa jambo hili la kuweza kuapa hapa mbele yetu.”

“Asubuhi ya leo ameapa kuwa mbunge kule bungeni. Alipofika ilibidi nimuhoji kidogo, unatoka mkoa wa Lindi, akasema sitoki Lindi nikasema tuko salama,”  amesema Spika Ndugai huku akiibua furaha kwa wageni waliohudhulia kiapo hicho.

Amesema, “hata aliposhika kiapo, watu walikuwa kimya. Tunashukuru sana, yote yamepita salama na sisi tutawapeni ushirikiano wa kutosha kabisa.”

Baada ya kumaliza kuzungumza, uliwadia wasaha wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyeanza kwa kumpongeza Profesa Manya “tunamfahamu, kati ya mambo makubwa yaliyofanyika kwenye madini, una mchango wako.”

“Tumeupokea uteuzi wako kwa imani kubwa na utatumia uzoefu wako, kufanya mabadiliko ya sheria ndani ya Bunge na yeye akiwa mbunge,” amesema Majaliwa ambaye ni Mbunge wa Ruangwa Mkoa wa Lindi

Akiendelea kuzungumza, Majaliwa amesema “sitaki sana kuzungumzia aliyosema Spika, eneo hili si la mzaha mzaha sana, hata mimi nilipokuwa naapa, ukitamka unavuta nguvu, yaliyotokea si ya Lindi, tuendelee kumwombea kijana wetu, bado mheshimiwa Rais unaweza kuangalia angalia.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!