Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mwigulu amponda Lissu, Nyalandu mbele ya JPM 
Habari za Siasa

Mwigulu amponda Lissu, Nyalandu mbele ya JPM 

Spread the love

DAKTARI Mwigulu Nchemba, mgombea ubunge Iramba Mashariki Mkoa wa Singida kupitia CCM, ameanza kumchokonoa Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chadema na Lazaro Nyalandu, mbombea ubunge Singida Kaskazini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Akizungumza kwenye kampeni za Dk. John Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho katika Uwanja wa Bombadier mkoani Singida leo tarehe 1 Septemba 2020 amesema, wawili hao hawana uzalendo.

Bila kuwataja majina, Mwigulu alimnanga Nyalandu kwamba, alipokuwa waziri (Waziri wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne) alikuwa akienda Ulaya kunyoosha suti zake huku Lissu akisema amerejea nchini baada ya kupewa ‘advance’ (malipo ya awali).

Lissu ndiye aliyerejea nchini akitokea kwenye matibabu nchini Ubelgiji, ni baada ya watu wasiojulikana kushamabuliwa kwa risasi ‘Area D,’ jijini Dodoma tarehe 7 Septemba 2017.

Mara kadhaa Lissu alinukuliwa na vyombo vya habari akiwa ughaibuni, kwamba alishindwa kurudi Tanzania kwa kuwa sio sehemu salama kwake.

Lazaro Nyalandu, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, akizungumza na waandishi muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu 2020 kwa tiketi ya Chadema

“Wengine wanakuja hapa wanajifanya watoto wa Singida, hawana uzalendo hata na wana Singida. Kuna mmoja tulikuwa mawaziri wote, hata suti zake alikuwa anaenda kunyoosha Ulaya, hana uchungu na Singida.”

“Mwingine alisema Tanzania sio salama, sasa hivi amekuja sababu ‘advance’ amechukua baada ya uchaguzi tu atasema, Tanzania haiko salama, ataondoka,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria, amewataka Watanzania kumchagua Rais Magufuli.

“Ioneeni huruma Tanzania, wale wagombea wengine wote mimi nawafahamu na nikiangalia janja janja yao, naona hata ‘advance’ wamechukua, nchi yetu itauzwa mkimuacha Dk. Magufuli,” amesema Dk. Mwigulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!