Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu kuboresha sekta ya afya, nyongeza ya mishahara
Habari za Siasa

Lissu kuboresha sekta ya afya, nyongeza ya mishahara

Spread the love

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema, iwapo atapewa ridhaa ya kuwa rais jambo la kwanza atakalolipa kipaumbele ni sekta ya afya. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo amesema, jambo lingine ambalo linatakiwa kupewa kipaumbele ni sekta ya kilimo na ufugaji ili kuondokana na maisha ya umasikini licha ya wazalishaji wakubwa wa chakula.

Lissu ametoa kauli hiyo leo Jumamosi tarehe 8 Agosti 2020 alipokuwa akizungumza katika Ofisi za Chadema Kanda ya Kanda baada ya kutoka Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu za kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

Amesema, Serikali imeshindwa kutambua umuhimu wa watumishi wa sekta ya afya kwa kushindwakujali maisha yao licha ya kujisifu wanajenga majengo pamoja na ununuzi wa vifaa.

Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara amesema, Serikali itakayoongozwa na Chadema itaboresha maisha ya watumishi wa sekta ya afya kwa kwa kuboresha masilahi yao binafsi.

Tundu Lissu-Chadema

“Mimi nimetibiwa hapa nchini baada ya kupigwa risasi lakini wote mnajua hali halisi ya waganga wetu, manesi na watu wengine, lakini ukienda kwenye nchi za watu wengine watumishi wa sekta hiyo wanajaliwa sana kuliko jambo lolote,” amesema

“Kama mimi nitapewa ridhaa ya kuwa rais, nitahakikisha tunaboresha sekta ya afya na siyo kujenga majengo makubwa na mazuri tu na ununuzi wa vifaa bali kuboresha maisha ya watumishi hadi kwa mfagiaji ili mtumishi wa sekta ya afya anapokuwa kazini asiwaze kuwa kuna shida gani nyumbani,” amesema Lissu.

Lissu alipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma tarehe 7 Septemba 2017 baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana na siku hiyohiyo usiku alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Tarehe 6 Januari 2018, Lissu alihamishiwa tena nchini Ubelgiji kwa matibabu hadi aliporejea Tanzania Jumatatu ya tarehe 27 Agosti 2020.

Kuhushu ufugaji, Lissu amesema, haiwezekani serikali ya Chadema isiwasaidie wafugaji kwa kuwaacha waendelee kuwa masikini kama ilivyo sasa.

Lissu amesema, jambo la kushangaza serikali ya awamu ya tano, imekuwa ikishindwa kuwasaidia wakulima na wafugaji ambao ndio walishaji wakubwa wa chakula kwa watanzania.

Mgombea huyo amesema, iwapo Serikali ya Chadema itachaguliwa, itahakikisha inawaboreshea maisha mazuri wakulima na wafugaji ambao kwa sasa wamegeuzwa kuwa masikini wakutupwa.

Akizungumzia nyongeza za mishahara, Lissu amesema, inasikitisha kwa serikali ya Tanzania ambayo inaongozwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miaka mitano, watumishi wameshindwa kuongezewa nyongeza za mishahara yao.

“Suala la nyongeza ya mishahara lipo kisheria kwani kila mwaka kunatakiwa nyongeza za mishahara ili kuhakikisha wanafanya shughuli zao ziende vizuri. Serikali nitakayoiongoza, itawajali watumishi kwa maslahi yao,” amesema.

1 Comment

  • Mbona Mbowe alitibiwa nchini pamoja na viongozi wengine wa upinzani? Ni Lissu tu ndio madktari wetu washindwe na akimbilie Nairobi?? Muwe wakweli

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RUWASA yachongewa, yateketeza mamilioni kwa maji yenye magadi

Spread the loveSAKATA la ukosefu wa maji wilayani Momba mkoani Songwe limezidi...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

error: Content is protected !!