Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo: Membe ni mtaji kwetu
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo: Membe ni mtaji kwetu

Spread the love

BERNARD Membe, aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Waziri wa Mambo ya Nje Nje katika Serikali ya Awamu ya Nne, ni mtaji katika chama chetu. Anaripoti Hamis Mguta, Mafia…(endelea).

Hiyo ni kauli ya Nasir Abubakari, Katibu wa Uenenzi wa Chama cha ACT-Wazalendo wilayani Mafia alipozungumza na mwandishi wa MwanaHALISI Online.

“Membe ni mtu ambaye anaonekana kuwa na busara kubwa kwasababu tangu afukuzwe kwenye chama chake, ametumia muda mrefu kutafakari na wala hajakurupuka,” amesema.

Abubakari ambaye ni metia nia ya kugombea udiwani wa Kata ya Kiegeani, Mafia kupitia chama hicho katika uchaguzi wa Oktoba 2020, ameuambia mtandao huu kwamba wanamkaribisha Membe kwa mikono miwili.

“Nimesikia amerudisha kadi na kama atakuja ACT-Wazalendo, basi nami naungana na wakuu wangu wa chama Maalim Seif na Zitto Kabwe kwamba aje, akufanya hivyo atakuwa amefanya maamuzi ya busara na hekima.

“Naamini Membe ana mtaji wa watu, atakuja na mtaji ambao ametoka nao CCM, wao wamemfukuza uanachama lakini ni kumzalilisha tu, mtu ambaye ameshika nafasi mbakimbali katika serikali na amefanya mambo makubwa, kitendo cha kumfukuza sio cha kiungwana, tunamkaribisha aje tuitengeneze Tanzania yetu,” anasema Abubakari.

Hata hivyo, Abubakari amesisitiza kuwa, kitendo cha vyama vya upinzani kuungana katika uchaguzi wa mwaka huu ni jambo litakalounganisha nguvu, pia itasaidia kama ilivyokuwa mwaka 2015 wakati alipokuwa kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Anasema katika uchaguzi wa mwaka 2020 Membe akipewa nafasi ya kupeperusha bendera ya urais kwa umoja wa vyama vya upinzani kama ilivyokuwa kwa Lowassa mwaka 2015, upinzani utachukua nchi kama Malawi.

“Membe akija ni kuchukua serikali tu, kwasababu wananchi wanamuhitaji, Malawi yamefanyika upinzani unaongoza nchi kwanini sisi tushindwe? Tusitishwe ya kwamba kutakuwa na vurugu, hapana”. anasema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!