Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Viongozi ACT-Wazalendo watoa tamko dhidi ya Membe
Habari za SiasaTangulizi

Viongozi ACT-Wazalendo watoa tamko dhidi ya Membe

Spread the love

VIONGOZI wa mikoa mitano ya Chama cha ACT Wazalendo, wamemwomba Bernard Membe, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Tanzania, akubari ombi lao la kujiunga na chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi…(endelea).

Viongozi wa mkoa ya Lindi, Mtwara, Mkoa wa Kichama Selou na Pwani wamefikisha ombi hilo nyumbani kwake (Membe) Rondo Mkoa wa Lindi leo Jumanne tarehe 7 Julai 2020.

Ombi hilo wamelifikisha ikiwa ni siku moja imepita tangu Membe aliporejesha kadi yake ya uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ofisi za chama hicho, Rondo mkoani huko jana Jumatatu.

Membe alichukua uamuzi huo baada ya tarehe 28 Februari 2020, kamati kuu ya CCM, kutangaza kumfukuza kwa madai kwamba amekuwa na mwendo mbaya ndani ya chama hicho tangu mwaka 2014.

Wakati akirejesha kadi hiyo, Membe alisindikizwa na mamia ya wana CCM ambao nao walizirejesha kadi zao huku mwanasiasa huyo akiwataka kuwa wativu kwani kwa pamoja watajiunga na chama kingine cha siasa.

Membe alisema, atagombea urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 pasina kueleza kupitia chama gani cha siasa.

Leo Jumanne, viongozi hao wa ACT-Wazalendo walifika nyumbani kwa Membe kuzungumza nao lengo likiwa kumshawishi akubari kujiunga nao.

Isihaka Rashid Mchinjita, Mwenyekiti Mkoa wa Lindi na Mjumbe wa kamati kuu ndiye aliyesoma tamko kwa niaba ya wenzake.

Amesema, tarehe 30 Juni 2020, Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zito Kabwe akihutubia wanachama katika mkutano wa ndani uliofanyika Kilwa Kivinje, alikukaribisba (Membe) kujiunga na vyama vya upinzani ili kuongeza mshikamano kuhami demokrasia na kuleta mabadiliko ya utawala nchini.

Amesema, kwao wito huo ulikuwa ni hatua muhimu kuelekea mageuzi makubwa ya kisiasa nchini humo.

“Uamuzi wa Ndugu Bernard Membe kurudisha kadi ya CCM tumeupokea kwa matarajio makubwa.”

“Hii ni kwa sababu uamuzi huu unafungua milango kwa yeye kuchagua kujiunga na vyama vya siasa vya upinzani nchini ikiwa ataona inafaa,” amesema Mchinjita

Amesema, wao kama viongozi wa kisiasa wamekuwa wakifuatiloa kwa umakini, misimamo, muelekeo na mtazamo wake kuhusu demokrasia, haki na utawala wa sheria.

“Kwa hakika tunaamini hayo ndiyo yaliyokufanya ufukuzwe CCM. Hata hivyo, mambo haya uliyoyapigania ukiwa ndani ya CCM ni hitajio kubwa la taifa letu,” amesema

“Ni kwa msingi huo ndiyo maana sisi viongozi wa ACT Wazalendo mikoa ya Lindi, Mtwara, Selou na Pwani tumekuja hapa kukuomba ujiunge na chama chetu cha ACT Wazalendo,” amesema Mchinjita huku akishangiliwa na wenzake.

Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Mwenyekiti huyo amesema,”Chama chetu kimejipambanua kwa kupigania haki, demokrasia, utawala wa sheria, mashirikiano ya vyama vya siasa na wadau wengine ili kuleta mabadiliko ya kiutawala na kuhami demokrasia nchini.”

Mchinjita amesema,”kwa nini sisi? Pamoja na ukweli kuwa wewe ni kiongozi wa kitaifa na siku zote umepigania maslahi ya kitaifa, lakini pia unatokea kusini.”

Akihitimisha tamko hilo, Mchinjita amesema,”Tunaona fahari ikiwa sisi tutawaongoza wengine kukuomba uje kujiunga na chama hiki ili ushiriki mapambano ya kujikomboa ili kurejesha utawala wa sheria, haki na demokrasia nchini.”

“Ni matarajio yetu kuwa utatukubalia na kujiunga na ACT – Wazalendo,” amesema

Viongozi wengine ni; Abdallah saidi Mtalika – Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kichama wa Selou, Alphonce Andrea Hitu – Mwenyekiti wa ACT Mtwara na Mrisho Khalfani Swagara-Mwenyekiti Mkoa wa Pwani

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!