Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nafasi ya Gambo Arusha yajazwa
Habari za Siasa

Nafasi ya Gambo Arusha yajazwa

Mrisho Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini (CCM)
Spread the love

MKUU wa Mkoa wa Arusha sasa ni Idd Kimanta, ambaye awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli jijini Arusha. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Uteuzi huo umefanywa leo tarehe 21 Juni 2020 na Rais John Mafufuli.

Kabla ya uteuzi wa Kimanta le tarehe 21 Juni 2020, mkoa huo ulikuwa ukiongozwa na Mrisho Gambo ambaye ametumbuliwa Ijumaa tarehe 19 Juni 2020.

Katika taarifa yake, Mkurugeni wa Mawasiliano Ikulu, jijini Dar es Salaam Gerson Msigwa imeeleza, nafasi ya Kimanta (Monduli) sasa itashikiliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Edward Jotham Balele. Balale alikuwa Wizara ya Mambo ya Ndani Nchi.

Pia Rais Maguduli amemteua Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, baada ya Rigina Chonjo, aliyekuwa akiongoza wilaya hiyo kustaafu.

Msulwa alikuwa ofisa mwandamizi na mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!