Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG aichunguza TPA, Bunge latoa maagizo
Habari za Siasa

CAG aichunguza TPA, Bunge latoa maagizo

Bandari Dar es Salaam Tanzania
Spread the love

OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, imeanza ukaguzi maalumu kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa tarehe 22Mei 2020 bungeni jijini Dodoma na makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Aeshi Hilaly alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo, kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30  Juni, 2019.

Hilaly amesema, CAG ameanza ukaguzi huo, kufuatia changamoto za kimfumo na utendaji, zilizojitokeza katika mamlaka hiyo, ambazo zimebainishwa katika ripoti hiyo.

Changamoto hizo ni; upungufu katika mfumo wa makusanyo ya fedha ya bandari, yaliyosababisha tofauti ya kiasi cha  Sh. 2 bilioni, zisizofanyiwa usuluhishi, pamoja na hati za madai ya Sh. 1.8 bilioni, ambazo hazikupatikana wakati wa ukaguzi.

“Dosari katika usimamizi wa mikataba, ambapo katika mikataba 7 iliyokaguliwa, CAG alibaini kutokuwepo taarifa za maendeleo ya miradi, suala hili ni kinyume na matakwa ya Kanuni ya 243 (1) ya 10Kanuni za Manunuzi ya Umma (PPR) za mwaka 2013 kama zilivyorekebishwa mwaka 2016,” amesema Hilaly

Amesema, changamoto nyingine zilizobainika katika taarifa ya CAG kuhusu TPA ni, ukiukwaji wa kanuni za fedha za TPA, baada ya mamlaka hiyo kuruhusu ongezeko la deni wakati huduma za bandari zinatakiwa zilipwe kwa fedha taslimu.

Makamu mwenyekiti huyo wa PAC, ameishauri Ofisi ya CAG kukamilisha ukaguzi huo kwa wakati, ili kuokoa matumizi na mapato ya Serikali.

“Kutokana na changamoto tulizobainisha hapo juu, CAG ameifahamisha kamati kuwa, ameanza zoezi la ukaguzi maalum (Special audit) katika eneo la ununuzi, usimikaji na utendaji wa mifumo mbalimbali ya shughuli za TPA.”

“Ukaguzi huu ni muhimu ukakamilika kwa wakati ili uweze kusaidia udhibiti wa matumizi na mapato ya Serikali,” amesema Kaboyoka.

Pia, PAC imeshauri  TPA itekeleze matakwa ya Sheria ya Manunuzi ya Umma na kanuni zake katika usimamizi wa mikataba, ili kudhibiti upotevu wa mapato.

“Serikali izingatie mapendekezo ya ukaguzi huo maalumu pindi utakapokamilika ili kuboresha shughuli za TPA,” amesema Hilaly  ambaye ni mbunge wa Simbawanga Mjini kupitia CCM

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

error: Content is protected !!